Nchi

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuNchiPeopleSiasa
Ummy Mwalimu

Watu Maarufu Tanzania

Siasa

Ummy Mwalimu

Waziri wa TAMISEMI

Mwlm Ummy
Tarehe ya Kuzaliwa:
1973-09-05
Mahali pa Kuzaliwa:
Tanzania

Ummy Ally Mwalimu alizaliwa 5 Septemba 1973 ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama tawala cha kisiasa nchini Tanzania.

Amechaguliwa kuwa mbunge wa Viti Maalum vya Wanawake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 nafasi ambayo aliitumikia hadi mwaka 2015. Akarudishwa tena bungeni Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kupitia tiketi ya CCM Viti Maalum vya Wanawake 2015.

Mwaka 2017 aliteuliwa kuwa waziri katika Wizara wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Mwaka 2021 aliteuliwa na raisi wa sita wa Tanzania, mama Samia Suluhu Hassan kuwa waziri katika wizara ya Nchi Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

ELIMU

Ummy Mwalimu alihitimu elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe mwaka 1998.

Alitunukiwa shahada ya sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1998.

Mwaka 2001 alitunukiwa shahada ya uzamili ya sheria katika chuo kikuu cha Pretoria. Ummy Mwalimu amefanya kazi sehemu mbalimbali serikalini na katika mashirika yanayojihusisha na tafiti kuhusu sheria, uongozi unaozingatia Sheria na Utawala Bora.

SIASA

Ummy Mwalimu ameshika nafasi mbalimbali katika ulingo wa siasa. Mwaka 2015 alikuwa mjumbe wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na mwaka 2014-2015 alikuwa mjumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Mwaka 2015 alikuwa Naibu Waziri wa Sheria na Katiba mwaka 2014 hadi 2015.

Amewahi kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Mazingira na mwaka 2010-2014 alikuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto.

Pia Ummy Mwalimu amekuwa Mbunge kwa vipindi viwili 2010 hadi 2015 na mwaka 2015 hadi 2020 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi kupitia Viti Maalum kwa Wanawake.

Mwaka 2007-2015 Ummy alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Tanga na mwaka 2008 hadi 2015 alikuwa mjumbe wa Umoja wa Wanawake (UWT) Tanga. Mwalimu ameshika nafasi nyingi za uongozi katika chama na serikali.

MAPAMBANO DHIDI YA UVIKO-19

Ummy Mwalimu amepata umaarufu mkubwa kutokana na umahiri wake wa kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaotokana na virusi vya Corona, kwa jina la kitaalamu COVID -19.

Ugonjwa huu uliingia nchini Tanzania tarehe 15 Machi 2020 Ummy amechukua aliitisha mkutano na waandishi wa habari nchini kwa weledi mkubwa kabisa alizungumza na taifa kwa lengo la kupunguz ataharuki na hofu kwa wananchi.

Ummy amezingatia weledi na kanuni za kukabiliana na majanga, jambo ambalo limewawezesha Watanzania kuendelea kufanya kazi bila hofu. Hivi karibuni Mwalimu alisema kuwa ugonjwa wa korona umepungua na kuwataka Watanzania kuendelea na shughuli zao huku wakichukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo.

TAMISEMI katika Wizara hii, Ummy anafanya kazi kila kukicha, aanawazungukia wanachi nchini nkote kwa ukaribu, kwa kuwazungukia Watumishi wa Umma ngazi ya Serikali ya mitaa, kuwezesha mazingira bora ya kazi kwa walimu, wauguzi na kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora chini ya mikakati ya Wizara yake.

TanzaniaWeb