Nchi

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuNchiPeopleBurudani
Steven Kanumba

Watu Maarufu Tanzania

Burudani

Steven Kanumba

Historia ya Kanumba

Screen 0
Tarehe ya Kuzaliwa:
1984-01-08
Mahali pa Kuzaliwa:
Shiyanga
Date of Death:
2012-04-07
DECEASED

Steven Charles Kanumba alizaliwa 8 Januari 1984, mkoa wa Shinyanga alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka nchini Tanzania.

Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania.

Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi tu. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchini.

Maisha Steven alianza masomo yake katika shule ya msingi yaBugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui na baadae kupata uhamisho katika shule moja jijini Dar es Salaam iitwayo Dar Christian Seminary.

Alivyomaliza kidato cha nne akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Jitegemee ilioko huko huko Dar es salaam.

Kanumba ameanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya “90”. Ila kufahamika zaidi alianza mwaka2002 mara tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kama Kaole Sanaa Group.

Steven Kanumba alijibebea umaarufu mkubwa nchini Tanzanian amekuwa kipenzi cha wengi na amekubalika karibuni nchi zote za Afrika Masharikina maziwa makuu.

Kwa sasa ameanza kutangaza sanaa nchi za Afrika ya Magharibi ikiwemo Nigeriana pia Wanigeria wamependezewa na uigizaji wake hivyo kushirikiana pamoja naye katika filamu kadha wa kadha.

Filamu ambazo wameshawahi kushirikiana pamoja ikiwemo na ile yaDar to Lagos,She is My Sisterna nyingine ambazo bado zinajengwa.Baadhi ya filamu na Tamthilia Alizoshiki ni Tufani ,Johari ,Gharika ,3Baragumu ,Sikitiko Langu ,Johari ,Dangerous Desire ,Dar 2 Lagosi ,Cross my Sin ,Village Pastor Family Tears, Rudi Sehemu A na nyingine nyingi.

Kanumba alifariki tarehe 07 April 2012 habari zilianza kusambaa kuwa Kanumba amefariki, baadae ilikuja kujulikana kifo kilitokana na kujigonga au kugongwa na kitu kizito kichwani wakati akiwa na mpenzi wake Elizabeth “Lulu” Michael Kimemeta.

Lulu hatimae alifunguliwa mashtaka kwa kifo hicho. Msiba wa Kanumba ulikuwa mmoja wa misiba iliyoutingisha mji wa Dar es Salaam kuna watu husema watu 25,000 walihudhuria shughuli za kuaaga na kumzika marehemu ambaye alizikwa katika makaburi ya Kinondoni tarehe 10 April 2012.Steven Kanumba alifanya kazi kubwakatika tasnia ya filamu kati ya tuzo alizoshinda ni

*.2006 Best Actor of the Year *.2007 Best Actor in Tanzania Award *.2007/2008 Best Artist of the Year Award

Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasnia ya filamu Tanzania. Taifa limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa zaidi kupitia sanaa hii.

TanzaniaWeb