Nchi

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuNchiPeopleSiasa
Stergomena Tax

Watu Maarufu Tanzania

Siasa

Stergomena Tax

Waziri wa Ulinzi na Usalama

Tax Sreg
Tarehe ya Kuzaliwa:
1960-07-06
Mahali pa Kuzaliwa:
Tanzania

Stergomena Lawrence Tax amezaliwa 6 Julai 1960, amewahi kuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) hadi tarehe 31 Agosti 2021. Nafasi yake ilichukuliwa na Elias Mpedi Magosi ambaye ni raia wa Jamhuri ya Botswana kama katibu wa SADC.

ELIMU

Dr.Tax amesoma katika shule kadhaa za msingi nchini Tanzania. Alipata Shahada yake ya Biashara na usimamizi wa Fedha kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mnamo 1991, Kisha alipata Shahada ya Uzamili ya masuala ya usimamizi wa sera na uchumi mwaka 1995 na Daktari wa Falsafa katika Maendeleo ya kimataifa mwaka 2002 katika chuo kikuu cha Tsukuba huko nchini Japan.

KAZI

Alianza Kazi mwaka 1991, katika Serikali ya Tanzania ambapo alikuwa akihusika na masuala ya kutoa misaada pamoja na usimamizi katika Wizara ya Fedha hadi mwaka 2002. Amehudumu kama Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji kuanzia mwezi Januari mwaka 2006 hadi 2007.

Amewahi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka mwaka 2008 hadi 2013. Aliteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa SADC katika mkutno wa 33 wa Wakuu wa Nchi na serikali uliofanyika katika jiji la Lilongwe nchini Malawi. Na mnamo tarehe 10 ya mwezi Seotemba mwaka 2021, chini ya Serikali ya wamu ya sita, inayoongozwa na Rais Samia, Dr.Tax anateuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika nafasi Kumi za ubunge anazoteua Rais. Ameapishwa na Spiaka Job Ndugai na kuwa Mbunge rasmi siku ya Ijumaa tarehe 10 mwezi septemba mwak 2021. Tarehe 12 septemba, siku kadhaa tu baada ya kuteuliwa kuwa Mbunge, Dr.Tax anateuliwa tena kuwa Waziri wa Ulinzi akichukua nafasi ya Marehemu Elias Kwandika.

TanzaniaWeb