Nchi

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuNchiPeopleMkuu wa Nchi
Samia Suluhu Hassan

Watu Maarufu Tanzania

Mkuu wa Nchi

Samia Suluhu Hassan

Rais

PICHA YA RAIS SAMIA
Tarehe ya Kuzaliwa:
1960-01-27
Mahali pa Kuzaliwa:
Tanzania

MAISHA YAKE

Mhe. Samia Suluhu Hassan alizaliwa Januari 27, 1960 katika Kijiji cha Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja. Ameolewa na Bw. Hafidh Ameir na wamejaaliwa watoto wanne, watatu wa kiume na mmoja wa kike.

ELIMU NA MAFUNZO

Mhe. Samia Suluhu Hassan alipata elimu ya msingi katika shule mbalimbali, zikiwemo Shule ya Msingi Chwaka iliyoko Unguja kuanzia 1966 hadi 1968, Shule ya Msingi Ziwani mwaka 1970 na Shule ya Msingi Mahonda mwaka 1972. Baada ya hapo, alijiunga na Shule ya Sekondari ya Ng’ambo kwa ajili ya masomo ya Kidato cha Kwanza hadi cha tatu, na Shule ya Sekondari Lumumba kwa ajili ya Kidato cha Nne kati ya mwaka 1973 hadi 1976.

Mwaka 1983, alipata Astashada katika Mafunzo ya Takwimu kutoka Chuo cha Uchumi, Zanzibar. Baada ya kufanya kazi kwa kipindi kifupi kwenye Wizara ya Mipango na Maendeleo, mwaka 1983 hadi 1986, alijiunga na Chuo cha Maendeleo ya Uongozi Mzumbe (IDM) kwa ajili ya masomo ya juu katika Utawala wa Umma. Aidha, alipata mafunzo mbalimbali katika Taasisi ya Chuo cha Utawala wa Umma Lahore, Pakistan 1987, Taasisi ya Eastern and Southern African Management Institute (ESAMI) 1991, na Taasisi ya Uongozi ya Hyderabad India 1998 kwa ajili ya Astashahada ya Utawala. Baada ya hapo, alijiunga na Chuo Kikuu cha Manchester kilichopo Uingereza kwa ajili ya masomo ya Juu ya Uchumi. Vilevile, alipata Shahada ya Uzamili ya Maendeleo ya Jamii kupitia programu ya pamoja kati ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Chuo Kikuu cha Southern New Hampshire, Marekani.

UZOEFU NDANI YA SERIKALI

Mhe. Samia Suluhu Hassan ni Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Aliapishwa Machi 19, 2021 kufuatia kifo cha ghafla cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Ndugu Samia ni mwanamke wa kwanza nchini kushika nafasi za Makamu wa Rais na hatimaye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nyadhifa nyingine alizoshika ndani ya Serikali ni; Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia mambo ya Muungano 2010/2015; Waziri wa Utalii, Biashara na Uwekezaji katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar 2005/2010 na Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira, Maendeleo ya Wanawake, na Watoto, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 2000/2005. Mwaka 2014, alihudumu kama Makamu Mwenyekiti wa Bunge lililojadili Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuandaa rasimu ya Katiba mpya ya Tanzania. Mwaka 1987 hadi 1988, alikuwa Afisa Mipango Rasilimali Watu na Mwaka 1977 hadi 1983, Karani Masijala.

UZOEFU NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Mhe. Samia Suluhu Hassan aliingia katika siasa kama mwanachama wa CCM tarehe 10 Juni, 1987. Aliingia katika siasa za uchaguzi mwaka 2000 katika nafasi ya Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar kama Mwakilishi wa Viti Maalum vya Wanawake hadi mwaka 2010. Kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, aligombea na kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwakilisha jimbo la Makunduchi, Zanzibar.

Mwaka 2002, alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, na vile vile, kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi; nyadhifa ambazo ameendelea kuzifanyia kazi hadi leo. Ndugu Samia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja; na alikuwa Mjumbe wa Kamati za Siasa Mkoa na Wilaya ya Kusini Unguja.

Kwa upande wa Jumuiya za Chama cha Mapinduzi, Ndugu Samia ni mwanachama wa Jumuiya ya Wanawake wa Tanzania (UWT) kuanzia mwaka 1996 hadi leo. Aidha, ameshiriki katika kuandika Ilani ya Chama cha Mapinduzi mara nne mfululizo kuanzia 2005/2010, 2010/2015, 2015/2020 na 2020/2025.

UZOEFU KATIKA TAASISI NYINGINE

Mwaka 2016, Mhe. Samia aliteuliwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Ban Ki Moon, kuwa Mjumbe wa Jopo la Umoja wa Mataifa kuhusu Uwezeshaji wa Wanawake Kiuchumi, akiwakilisha Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika kati ya mwaka 2016 na 2017. Katika kipindi cha ujumbe wake, aliwasilisha mambo 27 kwenye Jopo hilo, ambayo Serikali ya Tanzania ilibainisha kama hatua za kimkakati kwa ajili ya kuweka mfumo endelevu wa kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.

Miongoni mwa matokeo ya kazi zake ni kusimamia uanzishwaji wa majukwaa ya uchumi ya wanawake nchini kwa lengo la kuwaunganisha wanawake wafanyabiashara wadogo na wakati kwenye masoko, hasa wanawake wanaoishi mipakani, kuwaunganisha na mikopo nafuu na kuhimiza mafunzo ya ujasiriamali; na kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kuanzisha kampeni ya kuongeza uwajibikaji katika kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto, maarufu kama “Jiongeze Tuwavushe Salama”.

Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (World Food Programme) mwaka 1988 hadi 1997. Vile vile, amefanya kazi katika Kamati, Bodi na Taasisi mbalimbali kama vile; Mjumbe wa Kamati ya Msamaha wa Wafungwa (Parole Committee) ya Zanzibar (2001- 2010), Mlezi wa Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Zanzibar (1997-2000), Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote – EOTF (1996-2000), Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Taasisi zisizo za Kiserikali Zanzibar (ANGOZA) 1995-2000, Mwanachama wa Lions Club Zanzibar (1991-1998), Mjumbe wa Kamati ya Uundaji wa Sera ya Elimu Zanzibar (1996) na Mwanachama Mwanzilishi wa Taasisi ya Kuchochea Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (1991-1994).

Samia Suluhu Hassani alianza safari yake ya elimu katika shule ya msingi Chawaka iliyopo kisiwani Unguja na baadae alihamia shule ya msingi Ziwani iliyopo kisiwani Pemba kabla ya kurejea kisiwani Unguja na kumaliza elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Mahonda.

Elimu ya Upili ama Sekondari aliisoma kati ya mwaka mwaka 1973 mpaka mwaka 1976 ambapo kama ilivyokuwa kwenye elimu ya msingi,Samia Suluhu Hassan alisoma shule mbili tofauti ambapo alisoma kidato cha kwa nza mpaka cha nne katika shule ya sekondari ya Ngambo iliyopo visiwani Unguja kati ya mwaka 1973-1975 kabla ya kuhamia sekondari ya na Lumumba, iliyopo kisiwani Unguja mnamo mwaka 1976 ambapo alihitimu kidato cha nne.

Baada ya kumaliza elimu ya Sekondari,Samia Suluhu Hassan hakujinga moja kwa moja na masomo ya Chuo,kwani mwaka 1977, Aliajiriwa kama mchapishaji katika serikali ya Zanzibar ambapo alipanda mpaka ngazi ya kuwa afisa wa mipango serikalini kati ya 1987 na 1988.

Wakati akiwa mtumishi katika serikali ya mapinduzi ya Zanzibar,Samia Suluhu Hassan alikuwa akijiendeleza kielemu ambapo alisoma kozi fupi mbali mbali ikiwemo ya sheti ya takwimu kabla ya kujiunga na Taasisi ya Maendeleo na Uongozi ya Mzumbe Morogoro ambapo alihitimu stashahada ya juu ya Utawala mnamo mwaka 1986.

Kati ya mwaka 1992 mpaka 1994 Samia Suluhu Hassan alisoma stashahada ya Uzamili ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Manchester kilichopo nchini Uingereza.

Kiu ya Mama Samia Suluhu Hassan kujiendeleza kielemu haijawahi kufikia ukomo kwani mwaka 2015 alihitimu shahada ya uzamili katika maendeleo ya uchumi ya jamii katika program ya ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Chuo kikuu cha Southern New Hampshire cha nchini Uingereza.

Samia Suluhu Hassan aliolewa miaka miwili tu baada ya kuhitimu elimu yake ya sekondari kule visiwani Zanzibar mnamo mwaka wa 1978, ambapo alifunga pingu ya maisha Bw Hafidh Ameir, ambaye wakati huo alikuwa afisa wa Kilimo katika serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ambapo Wawili hao wamejaliwa watoto wanne ambapo Mmoja kati ya wanawe Wanu Hafidh Ameir aliyezaliwa mwaka 1982 ndiye anayefata nyayo za mama yake kwani , ni mwakilishi maalum katika bunge la Zanzibar.

Samia Suluhu Hassan mbali na kuhudumu Serikalini tangu amalize masomo yake ya sekondari akiwa na miaka 16 alipata kufanya kazi na mshirika ya kimataifa ambapo kati ya Mwaka 1992 mpaka mwaka 1994 alifanya kazi na shirika la umoja wa mataifa la mpango wa Chakula ambapo alihudumu kwa nafasi ya Afisa Miradi,Mbali na kufanya kazi Serikalini na katika shirika la umoja wa mataifa,Simia alipata kufanya kazi na taasisi zisizo za kiserikali kwa miaka karibu kumi akijikita zaidi katika harakati za usawa wa kijinsia

Bi. Samia alijiunga rasmi na siasa mwaka wa 2000 Alijiunga rasmi na siasa mwaka wa 2000 wakati alipochakuliwa kwenye baraza la wawakilishi la Zanzibar kama mjumbe maalum.,kuingia kwake kwenye siasa kuliifanya nyota yake kuanza kuchomoza katika medani za kisiasa na uongozi ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar baada ya akateuliwa kuwa waziri wa Afya, Jinsia na Watoto,uteuzi uliofanywa na Rais wa kipindi hicho Aman Karume.

Mwaka 2005 alichaguliwa tena kuwa mjumbe maalum na kuteuliwa upya kama waziri, wakati huu akipewa wizara ya Utalii, Biashara na Uwekezaji katika serikali ya visiwani..Mwaka wa 2010 alitia nia ya kuwania uwakilishi ambapo alichaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo la Makunduchi huko Zanzibar.

Nyota ya Samia ilivuka mipaka kwani mwaka muda mfupi baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 alichomoza kwenye baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuteuliwa na aliyekuwa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kuwa waziri wa maswala ya muungano katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akihudumu chini ya Makamu wa Rais Mohamed Gharib Bilal.

Machi mwaka 2014 Tanzania iliingia kwenye vuguvugu la kubadili Katiba yake ambapo huko nyota ya Samia ilichomoza tena ,baada ya kuchaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba mjini Dodoma. Bi Hassan alichaguliwa kwa kura 390 sawa na asilimia 74.6 na kumshinda mpinzani wake Amina Abdalla Amour ambaye alipata kura 126 sawa na 24%. Itakumbukwa Samia Suluhu Hassan wakati wa Bunge la Katiba kwani ndipo alipoanzwa kutabiriwa kushika nafasi ya juu zaidi ya kiutawala ambapo mmoja wa wajumbe aliwaasa wajumbe wamfikirie Mama Samia kwa nafasi ya juu zaidi kwenye uchaguzi uliokuwa unafuata wa mwaka 2015.

Nyota ya Samia Suluhu haikuwahui kuzimika wala kufifia kwani Julai mwaka 2015, Dkt John Magufuli mara baada ya mpambano mkali ndani ya CCM uliompa ushindi wa kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchauzi Mkuu wa mwaka huo,mbele ya wajumbe wa mkutani Mkuu alimpendekeza Mama Samia kuwa mgombea mwenza wake na hatimaye baada ya uchaguzi Samia Suluhu Hassan aliweka historia nyingine ya kupanda katika siasa za Tanzania kwa kwa chama chake kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu uliomuweka Samia katika historia nyingine ya kua msaidizi mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maana ya Makamu wa Rais.

Mwaka 2020, aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli wakati akiomba ridhaa ndani ya Chama chake ili apeperushe tena bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huo, kwa mara nyingine alimpendekeza Samia Suluhu kuwa mgombea mwenza wake ambapo ushindi wa chama chake uliilinda historia ya Mama Samia.

Samia amekuwa Rais wa Sita baada ya Julius Nyerere, Ally Hassan Mwinyi, Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli, ambapo ameapishwa kushika nafasi hiyo ya juu kabisa ya kiutawala na kiuongoza baada ya kukidhi matakwa ya Katiba ya Tanzania. Huyu ndiyo Samia Suluhu Hassan, mwenye haiba ya ukimya, kutoka kufanya kazi kama Karani na sasa ameapishwa kuwa Rais wa kwanza Mwanamke wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

TanzaniaWeb