Nchi

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuNchiPeopleSiasa
Medard Kelemani

Watu Maarufu Tanzania

Siasa

Medard Kelemani

Mbunge wa Chato

Kelemaniwww
Tarehe ya Kuzaliwa:
1968-03-15
Mahali pa Kuzaliwa:
Tanzania

Medard Matogolo Kelemani, amezaliwa tarehe 15 mwezi March mwaka 1968. ni Mwanasheria pamoja na Mwanasiasa nchini Tanzania.

Ni mbunge wa Chato kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, jimbo alilokuwa anatoka Hayati Magufuli.

ELIMU

Alianza elimu ya msingi mwaka 1978 na kuhitimu mwaka 1984 katika shule ya Nyambogo, aliendelea na elimu ya sekondari kwa mwaka 1985 hadi mwaka 1988 katika shule ya Kahororo na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari Milambo mwaka 1989 hadi mwka 1991.

Alichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alipochukua shahada ya Sheria mwaka 1993 hadi mwaka 1996. mwaka 200 hadi 2002 alijiungana chuo cha Dudee kilichopo nchini Uingereza na kuchukua Shahada ya Uzamili katika Sheria ya Madini na Nishati.

Mwaka 2000 hadi 2006 alisoma Shahada ya Uzamivu katika chuo kikuu cha Bedford cha nchini Uingereza, wakati huo alichukua masomo ya sheria kwa ujumla.

KAZI

Kazi yake ya kwanza ilikuwa katika Wizara ya Nishati na madini, aliajiriwa kama Afisa Sheria Mwandamizi, hii ilikuwa mwaka 1999 hadi mwaka 2006.

Mwaka 1999 pia alikuwa akifanya kazi na shirika la Shirika la Kimataifa la kushghulikia Wakimbizi UNHCR kama Mwanasheria.

Mwaka 2007 aliajiriwa katika ofisi ya Millenium Challenge Tanzania (MCC), alihudumu kama Wakili Mkuu wa taasisi hii.

Mwaka 2013 hadi 2015 alikuwa akitumika katika Wizara ya Nishati na Madini, kama Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria.

SIASA

Kwa wakati huu wote, Medard alikuwa ni Mwanachama hai wa chama cha Mapinduzi, hili linathibitika kwa yale aliyoyafanya katika chama hiki.

Mwaka 1986 hadi 1988, alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) katika jimbo la Kahororo.

Akiwa mwanafunzi alipewa madaraka na CCM ya kuwa Katibu Mkuu wa umoja wa vijanna Mkoa wa Tabora kuanzania mwka 1989 hadi 1991.

Kutokana na uzoefu wake mkubwa alioupata kwa kufanyakazi muda mrefu katika Wizara , mambo hayakuwa magumu kwake kipindi alipoonesha nia yakutaka kugombea rasmi.

Mwaka 2015 aligombea ubunge kwa tiketi ya CCM, katika jimbo la Chato, jimbo alilokuwa anatoka mgombea urais wa awamu ile Hayati Magufuli.

Alishinda kinyang'anyiro hicho na kuibuka mshindi na kubeba dhamana ya kuwawakilisha wananchi wa Chato.

Kutoka mwka 2015 hadi 2020 alikuwa alikuwa ni Mjumbe wa kamati ya Wizara ya Nishati na Madini,wakati huo huo akiwa Naibu waziri wa Nishati na madini hadi mwaka 2017 alipoteuliwa na Hayati Magufuli kuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Mwaka 2020, aligombea tena Ubunge katika jimbo la Chato na kushinda tena kwa nafasi nyingine, aliendelea kubaki katika Wizara ya Nishati na Madini hadi uteuzi wake ulipotenguliwa mwaka 2021 na Rais Samia.

Hadi kutenguliwa, kiongozihuyu aliweza kuwaongoza ujumbe wa Tanzania Nchini Morocco kwa mwaliko wa Waziri wa Madini na Maendeleo ya Nishati wa Morocco katika Mkutano wenye lengo la kukuza ushirikiano katika sekta za Nishati na sekta ya madini baina ya nchi hizi mbili.

Ziara hii ianfuata baada ya Mfalme wa Morocco kuja nchini mwkaa 2016 aliyeonesha nia ya kukuza ushirikiano bain aya nchi yake na Tanzania katika kuboresha Nishati.

Tunayaona mapinduzi mengi yaliyoanywa katika Wizara hii, kwa kuwezesha umeme kufika vijijini maarufu kama umeme wa 'REA'.

TanzaniaWeb