Nchi

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuNchiPeopleSiasa
Kingunge Gombale Mwiru

Watu Maarufu Tanzania

Siasa

Kingunge Gombale Mwiru

Mwanasiasa

Kingunge Late2
Tarehe ya Kuzaliwa:
1930-05-30
Mahali pa Kuzaliwa:
Tanzania
Date of Death:
2018-02-02
DECEASED

Kingunge Gombale Mwiru, alizaliwa mwaka 1930 tarehe 30 mwezi Mei, na kufariki tarehe 2 mwezi Februari mwaka 2018, katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu mara baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake.

Alikuwa ni mtu mwenye itikadi za komunisti za kuamini katika umiliki wa pamoja, imani ambayo inaelezwa aliisimamia kwa kipindi chote cha maisha yake licha ya mambo kubadilika ama tuseme zama kubadilika.

Aliamini katika mtazamo wa Marxian, akiamini kuhusu mgawanyo wa madaraka na kazi kuwa ndio unao zaa matokeo chanya katika jamii.

Licha ya kubatizwa katika kanisa katoliki, Kigunge yeye hakuwa ana amini sana katika dini japo aliheshimu dini zote, mara zote alipokuwa akiapishwa alikuwa akitumia Katiba ya nchi na sio vitabu vitakatifu kama wengine walivyokuwa wakifanya, yote ni kwa sababu alikuwa haamini katika dini.

Akiwa shule ya msingi darasa la sita, alitengwa na kanisa lake la Romani Katoliki kwa sababu alijulikana kuwa na itikadi za ukomunisti, hii ilimletea shida hadi shuleni.

ELIMU

Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Mchikichini kisha akajiunga na Shule ya Sekondari African Special na baadaye Shule ya Wavulana ya Tabora.

Akiwa mwanafunzi alipendelea sana kusoma vitabu wenzake walimpatia jina la 'thinker'

Akiwa shuleni alijiunga na chama cha TANU, wakati huo akiwa Tabora boys, akawa mwanachama rasmi wa chama hiko, na kw ahakika hakikumuacha patupu.

Mwaka 1958 alipelekwa na TANU nchini Liberia kwenda kusoma masomo ya Falsafa, nafasi hii alipewa na wenzake watatu, akiwa huko alianzisha harakati kali zilizopelekea uongozi wa chuo kutaka kumfukuza.

Licha ya kuwa na ufaulu ambao ungemwezesha kujiunga na Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda lakini alikataa kwenda huko na kutaka kwenda kusomea sheria nchini India.

Alikuwa Mwafrika wa Pili kuwa mkuu wa Chuo cha Kivukoni ambacho sasa kinajulikana kama Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambacho kilikuwa mahsusi kwa ajili ya kupika viongozi.

SIASA na KAZI

Kingunge alikuwa moja kati ya waasisi wa Chama cha Mapinduzi CCM wakati huo kikiitwa TANU,wanaotajwa kuwa waanzilishi wa chama hicho, alijitoa kwa hali na mali katika kukipigania chama chake.

Lakini pia ni muasisi wa kupigania uhuru wa Tanzania kwa wakati huo ikiitwa Tanganyika

Alikuwa ni kiongozi na mwanachama hai wa TANU.

Aliongoza harakati za kukiunganisha chama cha TANU na kile cha Afro shiraz Party ASP cha Zanzibar kilichounda chama cha Mapinduzi CCM, tarehe 5 ya mwaka 1977.

Toka kuwa kijana alitumikia taifa kwa kushika nyadhifa mbali mbali za juu katika serikali.

Ni miongoni mwa wajumbe wa kwanza wa kamati iliyoundwa na Mwalimu Nyerere kutengeneza mwongozo uliounda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadaye Katiba ya Zanzibar.

Ameshiriki kwa miaka mingi kutunga Ilani ya Uchaguzi ya CCM, ambayo ndiyo ahadi ya wagombea ubunge, udiwani, uwakilishi na urais wa pande zote za Muungano wanapokwenda kuomba kura kwa wananchi.

Alishiriki kuandika ilani za uchaguzi za CCM za mwaka 1995, 1990, 2000 na 2005.

Lakini hakuishia kwenye siasa tu, Kingunge alikuwa mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba mwaka 2014, akiwakilisha kundi la waganga wa jadi na tiba asili.

Aliajiriwa na Idara ya Public Waste (Wizara ya Ujenzi sasa) kama karani, mwaka 1954 Chama cha TANU kilizaliwa na wiki moja baadaye alijiunga na chama hicho.

Ili aelekeze nguvu zake zote katika kupigania Uhuru aliamua kujiuzulu nafasi yake ya ukarani mwaka 1956 na kutumika kama Katibu wa TANU.

Pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Pan African Movement ambapo alishika nafasi hiyo kwa muda mfupi kisha alirudi nchini na kuwa mwanasiasa.

Alikuwa Mwafrika wa Pili kuwa mkuu wa Chuo cha Kivukoni ambacho sasa kinajulikana kama Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambacho kilikuwa mahsusi kwa ajili ya kupika viongozi.

Alishika nafasi mbalimbali nchini zikiwamo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mbeya, Tanga, Mbunge Jimbo la Kilwa, Mjumbe wa Kamati Kuu CCM na Waziri katika wizara mbalimbali kwa nyakati tofauti.

Alikuwa Mshauri wa Rais katika masuala ya siasa hadi mwaka 2010 na pia alikuwa mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba akiwakilisha kundi la Tiba Asili.katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

KUONDOKA CCM

Alitangaza kuachana na chama hicho ikiwa zimebaki siku chache tu kufanyike uchaguzi mkuu nchini Tanzanzania octoba 25.

Kingunge alisema amefikia uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na utaratibu mzima wa uteuzi wa mgombea wa chama cha CCM na viongozi wake kukaa kimya bila kutoa maelezo.

Aidha alidai ukiukwaji wa huo, ulikuwa kinyume cha Katiba ya Chama hicho.

KUJIUNGA UKAWA Katika kampeni za urais za mwaka 2015, alijiunga na vyama vya Upinzani ambavyo kwa wakati ule viliungana kwa kushinikiza Katiba Mpya, umoja huo ulijulikana kama UKAWA.

Kingunge alisimama na kumnadi Edward Lowassa, aliyetimikia UKAWA, baada ya jin alake kukatwa katika mchakato w akura za maono katika Kamati kuu ya CCM.

Mwaka 2016, aliitisha mkutano na waandishi wa habari, alipowaomba Wazee wa CCM, kumshauri Hayati Magufuli, kuitisha kikao na viongozi wa CHADEMA kujadili kuhusu mwenendo wa siasa.

Hadi umauti unamkuta, Kingunge alikuwa hajarejea CCM, wala hakutaka kutambulika kama muumini wa chama chochote cha siasa nchini.

Alama aliyoiacha ya utumishi bora, ni chachu kwa viongozi wote wa umma kuifuata.

TanzaniaWeb