Nchi

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuNchiPeopleSiasa
Joseph Osmund Mbilinyi

Watu Maarufu Tanzania

Siasa

Joseph Osmund Mbilinyi

Historia ya Joseph Mbilinyi

Suguu
Tarehe ya Kuzaliwa:
N/A
Mahali pa Kuzaliwa:
Mtwara

Jina lake kamili ni Joseph Osmund Mbilinyi. Alizaliwa Mei mosi mwaka 1972 katika

hospitali ya Mkoa ya Ligula mkoani Mtwara. Baba yake aliitwa Osmund Mbilinyi na

mama yake aliitwa Desderia Lungu Mbilinyi. Katika familia yao amezaliwa na ndugu

kadhaa, wakiwemo Tryphone, Hartmann,Marysponsa, Gasper,Faustine,Emili na

Osmund.

Kwa kuzaliwa Mei Mosi ina maana kuwa Joseph alikuwa amezaliwa siku ya kimataifa

ya wafanyakazi duniani. Hivyo hakushangaza inaposemekana kuwa hatua ya kuzaliwa

siku hiyo akajulikana kwa jina la Mei.

Rekodi za historia zinaonesha kuwa alikuwa maarufu kwa jina la Mei. Licha ya kuanza

maisha ya utotoni akiwa Mtwara, ambako alihamia kuishi na bibi yake, baadaye

alihamia jijini Mbeya ambako alisoma shule ya msingi Sisimba.

Aidha, amewahi kuishi jijini Dar es salaam ambako alikuwa anasoma shule ya msingi

Sokoine iliyopo Temeke. Mwaka 1988 alijiunga na shule ya kutwa ya sekondari ya

Mbeya (Mbeya Day) ambako alisoma kidato cha kwanza hadi cha tatu ambako

aliposimamishwa kwa kosa la kukataa adhabu hadharani. baadaye alihamishiwa shule

sekondari Sabasaba mkoani Mtwara.

maisha ya ujana na ukubwani aliyaweka jijini Mbeya. Huko ndiko shughuli zake

zilizkoanzia na kuimarika hadi alipokuja kuingia katika siasa za vyama vingi mwaka

2010 kupitia Chadema.

MUZIKI

Kabla ya kujishughulisha na muziki, Joseph alifanya kazi mbalimbali ili kupata fedha

za kujikimu ikiwemo kuwa mlinzi.

tika historia ya muziki wa Bongofleva ndiko jina la Joseph Mbilinyi lilikonawiri zaidi.

Mbilinyi alianza muziki akiwa miaka 1990 akijiita jina la 2Prouds. Harakati zake za

muziki zilianzia akiwa mwanafunzi wa Mbeya Day, ambako alikuwa memba wa kundi

la BVSMP akiwa na marafiki zake Gibbon a Bonny.

Baada ya kuhitimu masomo yake alikuwa kwenye harakati za muziki ambako

alifanikiwa kujihusisha na makundi mbalimbali akiwa jijini Dar es salaam kabla ya

kurejea Mbeya. Alipokuwa Mbeya aliungana wenzake BBG na Sande kuunda kundi la

Niggaz 2 Public.

Ni kipindi amabcho wanamuziki wengi wa Bongofleva walikuwa wanatumia ala za

muziki za Marekani lakini wakighani mashairi ya Kiswahili. Katika hatua za mwanzo

za muziki alikuwa ameshiriki mashindano mbalimbali ya muziki jijini Dar es salaam

akishirikiana na Dar Young Mob kwenye mashindano ya Yo Rap Bonanza yaliyokuwa

yakiandaliwa na promota maarufu wakati huo Kim kupitia kampuni yake ya Kim and

The Boyz.

Katika vipindi tofauti ametoa albamu zake za muziki. Albamu yake ya kwanza alitoa

mwaka 1996 iliitwa ‘Ni mimi’. Mwaka 997 alitoa albamu ya ‘ndani ya bongo’. Mwaka

1998 alitoa albam nyingine ‘niite mr II’ kipindi hicho alikywa anaacha jina la 2prouds na kuanza kutumia jina la mr.2.

Mwaka 1999 alitoa albamu ya ‘Nje ya Bongo’ ambayo alitanagza kuwa alirekodia

nchini Uholanzi. Mwaka 2000 alitoa albamu nyingine iliyotwa ‘Milllenium’ ikiwa na

nyimbo nyingi kali na zilizosisimua wapenzi wa muziki kipindi hicho.

Mwanzoni mwa miaka 2000 alibadilisha jina lake kwa mara ya pili kutoka Mr 2 hadi

Sugu. Na sasa anajulikana kwa jina la Sugu kwenye majukwaa ya muziki.

SIASA

Mwaka 2010 Joseph Mbilinyi aliingia kwenye harakati za siasa. Sasa alikuwa

amebadilisha harakati kutoka kwenye muziki kwenda kwenye majukwaa ya siasa,

ambako alijiunganna CHADEMA.

Mwaka 2010 ulikuwa wa uchaguzi mkuu, ambapo aligombea ubunge wa Jimbo la

Mbeya Mjini kwa mara ya kwanza na kushinda. Uchaguzi wa mwaka 2015 alitetea kiti

chake cha ubunge wa jimbo hilo, lakini mwaka 2020 alishindwa kufurukuta mbele ya

mgombea wa CCM na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson Mwansasu.

BIASHARA

Katika biashara Joseph Mbilinyi anamiliki Hoteli Desderia iliyopo jijini Mbeya. Yeye ni mfanyabiashara ambaye alianza muda mrefu na hivyo alifanya harakati tatu za

biashara,siasa na muziki. Sugu amendelea kuwa mwekezaji ambapo miaka ya nyuma

alianzisha gazeti la burudani na michezo lililoitwa Deiwaka. Pia amechapisha matoleo

mawili ya vitabu vya historia ya maisha yake kutoka mitaani hadi kuwa mwakilishi wa

Bungeni.