Watu Maarufu Tanzania
- Tarehe ya Kuzaliwa:
- 1958-06-15
- Mahali pa Kuzaliwa:
- Tanzania
Jaji Prof.Ibrahimu Hamis Juma, amezaliwa mwaka 1958, tarehe 15 ya mwezi Juni katika Wilaya ya Musoma Mjini.
Amezaliwa katika hosptali ya Musoma mjini katika wodi ya Utawala ya Mukendo.
Kama anavyojulikana kwa taaluma yake ya Jaji, basi pasi na shaka ni lazima ana ubobevu mkubwa katika taaluma hii, lakini nikujuze machache kuhusu Jaji huyu Mkuu wa Tanzania.
ELIMU
Katika safari yake ya kujinoa katika sheria, Jaji huyu alianza mafunzo ya awali katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akichukua shahada ya sheria, akiwa chuoni hapo alifundishwa na Waziri Palamagamba Kabudi.
Alijiunga na chuo kikuu cha Ubelgiji akichukua masomo Islamic Law pamoja na Land Law, nafasi hii aliipata kwa kuteuliwa na uongozi wa Chuo Kikuu kutokana na uweledi wake katika masomo.
Hakuishia hapo tu, alipiga hatua kujiongezea tena elimu, wakati huu alichukua Shahada ya Uzamili katika Sheria ya Haki za binadamu katika chuo kikuu cha Raoul Wallenberg kilichopo nchini Sweeden.
Aliongeza tena elimu kwa kuchukua Shahada ya Uzamivu katika chuo kikuu cha Ubelgiji akichukua masomo ya Sheria ya Bahari.
KAZI
Mwaka 1980 hadi mwaka 1990 alipata nafasi ya kufundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anatajwa kuwa moja wa wafanyakazi waliofanya kazi kwa bidii, nidhamu na weledi mkubwa.
Ateuliwa kushika nafasi hii kutokana na uwezo wake mkubwa hasa nidhamu aliyokuwa nayo chuoni hapo, alipewa nafasi ya kuwa Mkuu wa kitivo cha sheria chuoni hapo.
Aliweza kubadilisha utaratibu wa kazi kwa kutengeneza mazingira rafiki kwa kila aliyekuwa chini yake, katika kipindi hiki aliweza kufanya kazi na Mwalimu wake, Pro.Palamagamba Kabudi, mara kadhaa Palamagamba amenukuliwa akisema sifa za Jaji huyu.
Anamtaja kama kiongozi asiye na ubaguzi mwenye kutii kila mtu pasipo kutazama hali ya kifedha ama uchumi wa mtu husika, hivi vitu vilifanya aweze kuongoza kitivo hicho kwa weledi mkubwa.
Baada ya kuhudumu kwa mwaka huu mmoja chuoni hapo, ndipo alipokwenda kufanya Shahada ya Uzamivu ya Sheria ya Bahari nchini Ubelgiji.
Jaji Prof Ibrahimu ni mwanazuoni mbobevu katika sheria za Bahari,ni kati ya wasomi wachache walioko Tanzania wenye utaalamu huo wa Sheria za Bahari akiwemo Prof Mahalu na Prof. Nasila Rembe kwa wale waliopitia vyuoni hasa upande wa sheria za Bahari,Haki za Binadamu,Sheria za Wakimbizi na Sheria za Mazingira wanamtambua Prof Ibrahimu kwa Machapisho na maandiko yake ambayo yanatumika na kila mwanafunzi.
Aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT), tume inayoshughulikia masuala yote ya mapitio ya sheria.
Wakati wote alikuwa akihudumu katika Mahakama kuu, na mwaka 2007 alipewa kazi ya kufatilia kuhusu mauaji ya wafanyabiashara watatu waliouwawa katika maeneo ya Sinza Dar es salaam. Aliifanya kazi hii akiwa chini ya Jaji Kipenka Mussa.
Mwaka 2008 aliteuliwa kuwa Jaji katika Mahakama Kuu ya Tanzania, nafasi aliyoitumikia kwa wedi mkubwa na haki, uongozi wake unatajwa kuwa wa haki kila anapokanyaga, kila anapopwewa nafasi ya kutumika basi hujibiidisha katika kutenda haki na usawa pasipo kutazamahali ya kimaisha ya mtu husika.
Mwaka 2012, alipandishwa cheo na kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaani.
Aliteuliwa na Hayati Magufuli kuwa Kaimu Jaji Mkuu kuanzia tarehe 18 Januari 2017 hadi alipoteuliwa kuwa Jaji Mkuu Tarehe 11, septemba 2017, alifanya kazi zote za Jaji Mkuu, kwa kuhidhinisha vikao vya Mahakama ya Rufaa, kusaini kanuni za kimahakama, na kuendesha vikao vya Tume ya Mahakama.
UTEUZI WA JAJI MKUU
Weledi wake katika Sheria umeleta mwanga mpya katika muhimili huu wa Mahakama aliapishwa kukaimu nafasi ya ujaji Mkuu wakati Taifa likikabiliana na vita dhidi ya Ubadhirifu,uhujumu uchumi vikiwemo vitendo vya ujangili, Rushwa na ukiukwaji wa Maadili kwa baadhi ya watendaji wa Umma kwa Kifupi Mtihani aliokuwa nao ni kurejesha imani kwa wananchi juu ya watendaji wa Mahakama kuzingatia Sheria, Haki na Wajibu.
Mwaka 2017, Septemba 12, aliapishwa rasmi na Hayati Maghufuli kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Ikulu ya Dar es Salaam, akipokea kijiti kutoka kwa Jaji Othman Chande.
Kwa taratibu za Mahakama, Nafasi hii huwa ni kwa kila baada ya miaka saba. Hotuba yake ya Kwanza akiwa kama Jaji Mkuu aliitoa mara baada ya kuapishwa, alisisitiza kuhusu misingi iliyowekwa na Majaji waliopita kuwa atahakikisha anaisimamia ili kuitunzia heshima Mahakama.
Katika utumishi wake hadi sasa, Jaji huyu ameweza kuwa mstari wa mbele katika kufanya mapinduzi ya undeshaji wa mashauri katika mahakama zote, amekuwa akipinga kuhusu mlundikano wa kesi, mahabusu, na masuala ya dhamana.
TanzaniaWeb