Nchi

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuNchiPeopleSiasa
Halima James Mdee

Watu Maarufu Tanzania

Siasa

Halima James Mdee

Historia ya Halima Dee

Mdeee
Tarehe ya Kuzaliwa:
N/A
Mahali pa Kuzaliwa:
Kilimanjaro
Date of Death:
1978-03-18
DECEASED

Halima James Mdee (alizaliwa Makanya, Wilaya ya Same, mkoa wa Kilimanjaro, 18 Machi 1978) ni mbunge wa viti maalumu katika bunge la Tanzania, lakini si tena kupitia chama pinzani cha CHADEMA.

Maisha Halima James Mdee ni mtoto wa mwisho katika familia ya Profesa James Mdee ambaye alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kikabila ni Mpare.

Mdee alizaliwa katika familia ya Wakristo na alibatizwa kwa kuitwa Theodosia, hata hivyo anatumia zaidi jina alilorithi kutoka kwa bibi yake mzaa baba, Halima. Ukoo wake ni waumini wa dini ya Kiislamu, isipokuwa baba yake na kaka yake ambao walibatizwa na familia yao ikaridhia wawe Wakatoliki.

Elimu Alianza kusoma elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Mlimani jijini Dar es Salaam mwaka 1985 na kuhitimu mwaka 1991. Alichaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari ya Wasichana Zanaki mwaka 1992 na kuhitimu kidato cha nne mwaka 1995.

Mwaka 1996 hadi 1998 alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kilakala mkoani Morogoro na 1999 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alisomea sheria na kuhitimu mwaka 2003. Aliendelea kusoma shahada ya uzamili ya sheria katika chuo kikuu cha Pretoria (Afrika Kusini) mwaka 2006 hadi 2007.

Kazi na siasa Alipata ajira katika Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana mwaka 2004 akiwa Ofisa Maendeleo kama mwanasheria mpaka mwaka 2005 alipoamua kuacha kazi na kuingia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, ambako alishiriki kuwapigia kampeni wagombea mbalimbali wa CHADEMA kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa viti maalumu.

Mwaka 2010 aligombea nafasi ya ubunge kupitia chama chake cha CHADEMA na alifanikiwa kupata nafasi hiyo. Halima alidumu nafasi hiyo kwanzia2010-2020. Aliendwa sana Wananchi wa kawe huku wakimpa maji tofauti kama Sauti ya Zege , Simba hakika alichuka taswira ya kuwa mwanamke hodari na mchapakazi.

Katika Uchaguzi wa mwaka 2020 alipogombea tena nafasi hiyo ya Ubunge jimbo la Kawe hakufanikiwa kupata, jimbo hilo limechukuliwa na Askofu.Josepht Gwajimaa kutoka chama cha Mapinduzi .

Kulingana na hali ya uchaguzi mwaka 2020 vyama pinzani vilika nafasi nyingi ya ugunge huku wakishutumu kuibiwa kura zao. ikapelekea mgogoro mkubwa kwa vyama pinzani na kuwakataza wenzao walibahatika kupata majimbo kukubali nafasi hizo.

Serikali ilipotoa nafasi maalum kwa vyama pinzani walimchagua Halima Mdee kua Mbunge wa viti maalum japo kuwa chama chake kilipinga nafasi hizo lakini Halima alikubali nafasi hiyo.

Ndipo chama cha CHADEMA kilipoambua kufuwafukuza uwanachama yeye na wenzake 9, Mpaka sasa halima ni mbunge wa viti maalum kutokea Chadema lakini huku chama chake hakimtambui kama mwanachama.

Vyeo vya chama Mbali na ubunge, pia alikuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la CHADEMA, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA na ofisa katika kurugenzi ya sheria.

TanzaniaWeb