Nchi

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuNchiPeopleMkuu wa Nchi
Dr. Philip Isdor Mpango

Watu Maarufu Tanzania

Mkuu wa Nchi

Dr. Philip Isdor Mpango

Makamu wa Rais

PHILIP MPANGO VP
Tarehe ya Kuzaliwa:
1957-07-14
Mahali pa Kuzaliwa:
Kigoma

Dr. Mpango ni mzaliwa wa Kigoma, baba yake ni marehemu Isidori Nzabhayanga Mpango, ambaye alizaliwa Kijiji cha Kasumo, Wilaya ya Kasulu.

Dkt. Mpango alizaliwa hapo hapo Kasumo na ni kaka mdogo wa Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanganyika Magharibi - Kasulu mkoani Kigoma, Dk Gerard Mpango.

Dk Mpango ni mchumi mwenye shahada ya uzamivu ya uchumi. Kuanzia miaka ya 1990 hadi 2000, alifanya kazi akiwa mhadhiri mwandamizi wa uchumi katika kitivo cha Biashara (sasa Shule ya Biashara) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Alikuwa akifundisha "Microeconomics", "Macroeconomics" (kwa mwaka wa pili) na "Public Finance" kwa mwaka wa tatu na kozi za uzamili. (Kwa tafsiri yangu, Uchumi mdogo, Uchumi mkubwa na masuala ya Fedha za umma.)

Amewahi kuwa Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Mkuu wa Kamati ya kumshauri Rais Jakaya Kikwete wakati huo kuhusu masuala ya uchumi, Katibu binafsi wa Rais anayeshughulikia masuala ya uchumi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, kabla ya kuhamishiwa Tume ya Mipango, Ofisi ya Rais. Nyadhifa hizi zote amezishika wakati wa utawala wa Kikwete. Hayati Magufuli alipoingia madarakani alimteua kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na baada ya siku chache akateuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Katika uchaguzi wa mwaka 2020 alishinda kiti Cha ubunge jimbo la Buhingwe. Kisha kuteuliwa tena kuwa waziri wa fedha na Mipango. Dk. Mpango hana tabia za kawaida unazoweza kuzihusisha na wanasiasa wa Afrika. Mpango ni msema kweli, mwadilifu, mcha Mungu na mtu ambaye anaamini katika vitendo kuliko maneno.

Sababu hizo, pamoja na uwezo wake kama mchumi, ndizo zilizomfanya abaki kuwa Waziri wa Fedha katika muda wote wa miaka sita ya utawala wa Rais Magufuli. Jambo hilo si dogo kwa sababu wizara hiyo ilikuwa ikiangaliwa kwa jicho la karibu na Rais Magufuli ambaye alijulikana kwa kutovumilia wateule wake ambao walionekana kutokidhi matarajio yake.

Dk. Mpango ni mwanasiasa wa bahati mbaya kwa sababu katika utumishi wake wa takribani miaka 40 serikalini, mara zote alitumika kama mtaalamu na aliingia kwenye siasa kwa kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa mbunge na baadaye waziri miaka sita iliyopita. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ulikuwa ni mara yake ya kwanza kuwania ubunge - bila shaka kwa kutosubiri tena kupata huruma ya Rais Magufuli ya kuteuliwa.

Bunge lilimthibitisha Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo jana baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwasilisha mapendekezo ya jina lake kuwa makamu wa Rais katika kikao maalumu cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Baadaye jina hilo kuwasilishwa bungeni na kupitishwa kwa kura 363 sawa na asilimia 100 ya kura zote zilizopigwa. Baada ya kupokea jina lake, Spika Job Ndugai alilitangazia bunge jina hilo lililopendekezwa na Rais Samia.

Mara baada ya tangazo hilo bunge lililipuka kwa shangwe. Bwana Mpango alikuwa waziri mwandamizi katika serikali ya hayati John Magufuli akihudumu kama waziri wa fedha. Na kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, asilimia 50 ya wabunge wanatakiwa kuukubali uteuzi huo ili kuthibitishwa.

Kabla ya jina hilo kuwasilishwa bungeni hii leo, kwanza liliwasilishwa katika Kamati kuu ya chama tawala CCM na kuthibitishwa. 'Nimepigwa na butwaa' Mara tu baada ya jina lake kusomwa Spika Ndugai alimpatia Mpango muda wa kujieleza ndani ya Bunge. Mpango akaeleza kuwa hakujua chochote juu ya uteuzi huo na kwamba alipigwa na butwaa.

''...Hii ni heshima kubwa sana, sikuwahi kuota (kama nitaipata)...Mpaka Naibu Waziri wangu akiwa anajibu maswali asubuhi hapa, nilikuwa nafikiria majukumu yangu yanayonikabili ikiwemo mishahara ya wabunge ambayo baadhi imechelewa mpaka asubuhi hii. Nimepigwa na butwaa..."

Taarifa za Serikali