Nchi

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuNchiPeopleSiasa
Asha Rose Migiro

Watu Maarufu Tanzania

Siasa

Asha Rose Migiro

Historia ya Asha Rose Migiro

Mom
Tarehe ya Kuzaliwa:
1956-07-09
Mahali pa Kuzaliwa:
Songea

Asha Rose Migiro alizaliwa Songea, Kusini mwa Tanzania mnamo tarehe 9 Julai mwaka 1956. Wazazi wake ni wenyeji wa mkoani Kilimanjaro ambako ndipo ilipo asili yake, na kabila lake ni Mpare.

Alianzia elimu yake ya shule ya msingi katika shule ya msingi Mnazi Mmoja iliyopo jijini Dar-es-salaam mwaka 1963 mahali ambapo aliposoma mpaka mwaka 1966 alipohamia shule ya msingi Korogwe iliyopo Korogwe,Tanga kuanzia mwaka 1967 hadi 1969 alipomalizia elimu yake ya msingi.

Kuanzia mwaka 1970 hadi 1973 hapo alijiunga na shule ya sekondari ya wasichana WeruWeru iliyopo Moshi,Kilimanjaro. Kwa elimu ya high school Dr.Migiro kuanzia mwaka 1974, alisomea katika shule ya Sekondari ya Korogwe iliyopo Korogwe,Tanga ambapo alihitimu mwaka 1975.

Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam mwaka 1977 kuchukua shahada ya kwanza ya sheria. Alihitimu mwaka 1980. Baada ya hapo alifanya kazi ya uwakili kwa muda mfupi. Kuanzia mwaka 1982 hadi 1984 Dr. Migiro alirejea tena katika Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam kwa ajili ya shahada ya pili ya Sheria (Masters).

Safari ya kimasomo ya Dr.Asha-Rose Migiro haikuishia hapo kwani mwaka 1988 alijiunga na Chuo Kikuu cha Konstanz kilichoko nchini Ujerumani kwa ajili ya masomo ya kutoka chuo hicho hicho kikuu cha Dar-es-salaam mnamo mwaka 1984. Baada ya hapo alikwenda nchini Ujerumani kusomea shahada ya udaktari wa falsafa (PhD) katika masuala hayo hayo ya sheria katika Chuo Kikuu cha Konstanz ambapo alihitimu masomo yake mwaka 1992.

Kabla ya kuelekea Ujerumani, kikazi tayari alikuwa ni mwajiriwa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa mkufunzi msaidizi mwaka kuanzia mwaka 1981 na baadaye, baada ya kurejea toka masomoni Ujerumani, kupanda katika ngazi za mhadhiri msaidizi, mhadhiri hadi mhadhiri mwandamizi, cheo alichokuwa nacho mpaka mwaka 2000 alipoingia kwenye siasa. Aliingia kwenye siasa na moja kwa moja kugombea ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa taasisi za elimu ya juu.

Baada ya kumalizika kwa uchaguzi, aliteuliwa na Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, nafasi aliyoishika hadi mwaka 2005.

Mnamo mwaka 2007 , Dr.Asha-Rose Migiro, aliteuliwa na Ban-Ki-Moon kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, umoja ulioanzishwa mnano mwaka 1945 na wenye makao yake makuu New York nchini Marekani. alisifika kwa mwanamama mchapakazi hodari na mahari katika maswala ya uchumi na jamii na mikakati bora ya madendeleo alidumu kwenye nafasi hiyo hadi mwaka 2012.

Mwaka 2015 alishriki kuchukua form ya kuwania nafasi ya urais lakini hakufanikiwa kupita nafasi hiyo ilichukuliwa na hayati.John Maghufuli.

Mei 2016, aliteuliwa na Rais wa awamu ya tano John Maghufuli kuwa balozi wa Tanzania nchini uingereza.

Huyo ndiye Asha-Rose Migiro mwanamke msomi mchapakzi mzuri amabaye afanya kazi nzuri sana kwenye nafasi zake za uwongozi na kuacha alama kubwa ikiwa ni pamoja na kusogeza gurudumu la maendeleo.

TanzaniaWeb