Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Volleyball

Staa wa mpira afariki kwa kuanguka ghorofani

Julia Ituma Julia Ituma

Fri, 14 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa mchezo wa Mpira wa Wavu (Volleyball) raia wa Italia, Julia Ituma amekutwa amefariki baada ya kuanguka kutoka ghorofani hadi chini kwenye hoteli masaa machache baada ya timu yake kutolewa katika hatua ya Nusu Fainali mjini Istanbul, Uturuki.

Ripoti zinaeleza kuwa Ituma alianguka kupitia dirisha la chumba ambacho alikuwa akikaa na rafiki yake kwenye ghorofa ya sita ya hoteli hiyo, ambapo alikutwa chini majira ya saa 11:30 asubuhi ya jana.

Ituma alizaliwa mwaka 2001 mjini Milan, wazazi wake wakiwa na asili ya Nigeria, aliaza kucheza mchezo huo akiwa na miaka 11.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live