Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Wimbledon yazuia wacheza tennis wa Russia

Wimbledon Tennis Wimbledon yazuia wacheza tennis wa Russia

Thu, 21 Apr 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Waandaaji wa michuano ya tennis ya Wimbledon wamezuia wacheza tennis wa Russia na Belarus kushiriki mashindani ya mwaka huu kutokana na uvamizi nchini Ukraine, lakini chama cha mchezo huo, ATP na cha wachezaji wanawake WTA vimesema hatua hiyo "si haki" na "inaudhi".

Waandaaji wa michuano ya Wimbledon ambao niĀ  All England Lawn Tennis Club (AELTC), walisema wamechukua hatua hiyo "kudhibiti ushawishi wa Russia kwa kutumia njia yoyote inayowezekana".

Mchezaji wa Russia anayeshika nafasi ya pili kwa ubora duniani kwa upande wa wanaume, Daniil Medvedev na mchezaji wa kike wa Belarus, Aryna Sabalenka, anayeshika nafasi ya nne duniani kw aubora na aliyefika nusu fainali ya Wimbledon mwaka jana, ni miongoni mwa wachezaji maarufu watakaozuiwa na uamuzi huo.

"Katika mazingira ya kitendo kama hicho kisicho cha haki na ambacho hakijawahi kutokea cha uvamizi wa kijeshi, haitakubalika kwa utawala wa Russia kunufaika na kuhusika kokote kwa wachezaji wa Russia au Belarus," taarifa ya AELTC imesema.

"Kwa kuangalia ukubwa wa mashindano hayo nchini Uingereza na duniani, ni wajibu wetu kutekeleza jukumu katika jitihada kubwa zinazofanywa na serikali, sekta, michezo na taasisi za ubunifu kudhibiti ushawishi wa Russia kupitia njia zozote zinazowezekana."

Chama cha Tennis kimepiga marufuku wachezaji wa Russia na Belarus kushiriki mashindano mengine yoyote ya viwanja vya majani, yakiwemo ya kujiandaa kwa Wimbledon ambayo hufanyika katika klabu ya Queen na Eastbourne.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz