Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Vipimo vya Djokovic ni halali

Novak Djokovic Walter Novak Djokovic

Thu, 3 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waendesha mashtaka nchini Serbia wamesema hakuna ushahidi wowote,unaoonesha kwamba Novak Djokovic amewasilisha vyeti vya uwongo vya majaribio ya Covid, kwa mamlaka ya Australia.

Vipimo hivyo vilitolewa ili kumwondolea Djokovic sheria, zinazowazuia watu ambao hawajachanjwa kusafiri.

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Umma wa Belgrade sasa imesema kuwa, Wizara ya Afya imethibitisha kuwa hati hizo ni za kweli.

Ofisi hiyo inasema ilikagua database ya kielektroniki ambayo ina maelezo ya vipimo na matokeo, na inaonesha kuwa kipimo cha awali cha Djokovic chanya na matokeo yake ya baadaye yalikuwa halali.

Kauli ya mwendesha mashtaka inakuja katika mkesha wa mkutano, kati ya mchezaji tenisi na Rais wa Serbia Aleksandar Vucic.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live