Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Tsonga atundika daluga

Tsonga Jo-Wilfried Tsonga

Wed, 25 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa mchezo wa tennis Mfaransa, Jo-Wilfried Tsonga ametangaza kustaafu mchezo huo baada ya kuondoshwa na Mnorway Casper Ruud kwa seti 6-7 (6-8) 7-6 (7-4) 6-2 7-6 na (7-0) kwenye michuano ya wazi ya Ufaransa (Frenc open 2022).

Tsonga mwenye umri wa miaka 37,amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya mguu tangu mwaka 2020,Amehitimisha miaka 18 ya kucheza mchezo wa tennis akishinda kwenye michezo 467 huku akijivunia kushika nafasi ya 5 kwa viwango vya ubora duniani kwa mchezo wa tennis.

"Leo ni siku kubwa kwangu ,siku ya kusema kwaherini na kuwashukuru watu wote mliokuwa nami kwenye safari yangu ya mchezo wa tennis na najiona mtu mwenye bahati kupata nafasi ya kuwa mmoja wa kizazi bora cha mchezo wa tennis kutoka nchini Ufaransa “ amesema Tsonga.

Nyota huyo ameshinda mataji 18 sambamba na kufika fainali mbili za Wimbledon na hatua mbili za nusu fainali ya michuano ya wazi ya Ufaransa pamoja na kutwaa taji la Davis Cup mwaka 2017.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live