Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Svitolina : Nilikuwa Katika Misheni ya Nchi Yangu.

TEEEEEEEEENI Elina Svitolina

Wed, 2 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mcheza Tenisi wa Ukraine, Elina Svitolina alifunga Mrusi Anastasia Potapova katika msahindano ya Monterrey Open huko Mexico hapo jana, na kusema anaweza kufanya mengi kwa ajili ya nchi yake kwa kucheza kuliko kugomea mechi hiyo.

Hapo awali Svitolina alikataa kucheza mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Potapova kwenye mashindano ya Monterrey Open, lakini akaendelea baada ya mamlaka ya tenisi kuamua kuwapiga marufuku wachezaji wa Urusi na Belarus kushiriki mashindano chini ya jina na bendera ya nchi zao.

“Leo ilikuwa mechi maalum kwangu,” Svitolina mwenye umri wa miaka 27 alisema. “Niko katika hali ya huzuni sana, lakini nina furaha kuwa ninacheza tenisi hapa.

“Nilizingatia. Nilikuwa kwenye misheni kwa ajili ya nchi yangu. Tangu mwanzo, ilikuwa muhimu kuwa tayari kwa lolote litakalonijia.”

“Nadhani ni dhamira yangu kuunganisha jumuiya yetu ya tenisi kusimama na Ukraine, kusaidia Ukraine kwa sababu tunayopitia ni jambo la kutisha kwa wote. Waukrainia.” aliongeza Svitolina.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live