Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Raducanu kuikosa michuano ya Wimbledon 2022?

RADUCANU Mcheza tennis, Emma Raducanu

Fri, 10 Jun 2022 Chanzo: eatv.tv

Mcheza Tennis anayeshika nafasi ya kwanza kwa Ubora nchini England, Emma Raducanu anataraji kuwa fiti na kushiriki michuano ya Wimbledon baada ya Uchunguzi wa kitabibu kuonesha jeraha lake halikuwa na madhara makubwa ya kumuweka nje kwa muda mrefu.

Bingwa huyo wa US Open wa mwaka 2021 alitangaza kuacha kucheza tennis kwa muda baada ya mechi yake ya kwanza kwenye michuano ya Nottingham siku ya jumanne baada ya kupata jeraha katika ubavu wake wa kushoto ambalo lilimlazimu kujitoa katika michuano hiyo.

"Imekuwa ni hali ya kusikitisha kulazimika kuondoka Nottingham wiki hii nikiwa na jeraha la ubavuni na kwa bahati mbaya pia sitaweza tena kucheza michuano ya Birmingham". Alisema Raducanu.

Licha ya majibu ya uchunguzi ya Jeraha hilo kuonyesha kutokuwa na madhara makubwa, lakini Raducanu hataweza kucheza katika hafla ya WTA itakayofanyika wiki ijayo katika viunga vya Birmingham.

Chanzo: eatv.tv