Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Raducanu amtamani Andy Murray

Emma Raducanu Nyota wa Tennis wa England Emma Raducanu

Tue, 7 Jun 2022 Chanzo: eatv.tv

Nyota wa tennis Muingereza Emma Raducanu amesema hana haraka ya kutafuta mkufunzi mpya baada ya kuachana na kocha wake Torben Beltz mnamo mwezi April mwaka huu huku akiwa ni mwalimu wake wa tatu kuachana naye ndani ya kipindi cha mwaka mmoja

Raducanu mwenye umri wa miaka 19 ambaye anashikilia taji la ubingwa wa michuano ya wazi ya Marekani (US Open) amesema ni mapema sana kufikiria kuhusu mkufunzi wake mpya huku tangu anyakuwe ubingwa wa US Open amekuwa akiandamwa na majeraha yaliyosababisha kutolewa mapema kwenye michuano mbalimbali aliyoshiriki kwa mwaka 2022.

Nyota huyo anayekamata nafasi ya 11 kwa viwango vya ubora duniani amesema ndoto zake za siku za mbeleni kucheza pamoja na Muingereza mwenzake Andy Murray kama timu moja kama ambavyo Murray alicheza na Serena Williams mnamo mwaka 2019

Chanzo: eatv.tv