Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Raducanu Atolewa BNP Paribas Open, India Wells

Skysports Tennis Emma Raducanu 5705435 Mcheza Tenisi wa Uingereza, Emma Raducanu

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mcheza Tenisi wa Uingereza, Emma Raducanu ametupwa nje ya mashindano ya BNP Paribas Open, Indian Wells baada ya kupoteza mchezo wake wa hatua ya 32 kwa seti tatu mbele ya Petra Martic wa Croatia.

Raducanu alikuwa akishiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza, alionekana kuwa kwenye mstari wa kutinga hatua ya 16 bora baada ya kushinda seti ya ufunguzi kwa sare ya 7-3.

Martic aliongoza tena katika seti ya pili, na kuchukua matokeo 6-4 na baadae Raducanu alionekana kupata uongozi tena kabla ya mapumziko na kushinda seti 5-4 kabla Mcroatia huyo kushinda mechi tatu mfululizo.

Baada ya ushindi wa Seti 7-5 Martic ataingia hatua inayofuata ambako atakutana na mchezaji namba 28 kwa ubora duniani, Liudmila Samsononova.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live