Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Nyota wa Tennis afungiwa miaka minne, kisa ni hiki..!

Miaka Minne Nyota wa Tennis na Bingwa wa zamani wa Wimbledon, Simona Halep

Wed, 13 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Tennis na Bingwa wa zamani wa Wimbledon, Simona Halep amefungiwa kujihusisha na michezo kwa miaka minne kutokana na makosa mawili ya matumizi ya dawa ya kuongeza uwezo.

Halep (31) kutokea Romania alisimamishwa tangu Oktoba mwaka jana baada ya majibu ya vipimo kuonyesha kuwa alitumia dawa kinyume na sheria.

Nyota huyo alishinda Ubingwa wa Wimbledon mwaka 2019 baada ya kumtoa Serena Williams kwenye Fainali.

Wakala wa Kimataifa wa uadilifu katika mchezo wa Tennis umethibitisha kuwa nyota huyo amefungiwa hadi Oktoba 6, 2026.

Halep amekana makosa hayo na kusema kuwa hakubaliani na kufungiwa kwa miaka minne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live