Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Novak Djokovic akiri kuvunja kanuni za kujitenga alipokuwa na Covid

Novak Djokovic Novak Djokovic

Wed, 12 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Novak Djokovic amekiri kukiuka sheria za kujitenga baada ya kupatikana na Covid-19 mwezi uliopita, na kuelezea kama "kosa la uamuzi".

Katika chapisho kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram siku ya Jumatano, Mserbia huyo alikiri kukutana na mwandishi wa habari kwa mahojiano siku mbili baada ya kupimwa na kuambukizwa mnamo 16 Desemba.

"Ninakubali kwamba nilipaswa kuahirisha mkutano huo wa mahojiano," aliandika.

Shughuli zake imechunguzwa huku serikali ya Australia ikizingatia iwapo itamfukuza nchini humo.

Katika ujumbe huo, pia alimlaumu wakala wake kwa kufanya makosa kwenye fomu ya usafiri aliyotumia kuingia Australia. Maoni yake yamesababisha uchunguzi mpya kutoka kwa maafisa.

Djokovic ambaye hajachanjwa anatarajia kutetea ubingwa wake wa Australian Open wiki ijayo.

Visa yake ilifutiliwa mbali mnamo 6 Januari muda mfupi baada ya kuwasili nchini huku kukiwa na maswali juu ya kutopokea chanjo ambayo ingemruhusu kuingia.

Lakini Mahakama imeruhusu kurudishwa kwa Viza hiyo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live