Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Novak Djokovic Kutetea Ubingwa Australian Open

Novak Djokovic Beats Daniil Medvedev 7 5 6 2 6 2 To Win Ninth Australian Open Title At Melbourne Par Novak Djokovic

Tue, 4 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuwepo sintofahamu kuhusu ushiriki wa bingwa mtetezi wa Australian Open, Novak Djokovic, sasa ni rasmi, ubingwa utatetewa kwa uwanjani.

Mashindano ya Australian Open yataanza Januari 17 jijini Melbourne, Australia. Kutokana na uwepo wa maambukizi ya virusi vya COVID-19, mamlaka za mji huo pamoja wa waandaji wa mashindano, walisema wazi, washiriki wote wanapaswa kuwa wamechanja au wawe na vielelezo vilivyothibitishwa na wataalamu kuwa wasichanje.

Mpaka sasa, Novak Djokovic hajaweka wazi nafasi yake katika mchakato wa kupata chanjo. Haijulikana kama amachanja au hajachanja. Lakini, imeripotiwa kuwa, Djokovic amepatiwa vielelezo vya kitabibu vitakavyo mruhusu kutetea taji lake la Australian Open.

Hii inamaana kuwa, Djokovic atashiriki mashindano hayo nchini Australia mwaka huu, 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live