Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

"Nilifanya maamuzi mabaya" - Andy Murray

ANDY MURRAY 2021 Mcheza tenisi wa Scotland, Andy Murray.

Fri, 22 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Mchezaji wa Tenisi, Andy Murray wa England, amekiri kuwa kupoteza umakini na kuzidiwa kimbinu na Diego Schwartzman, kumepelekea kupoteza mchezo wa hatua ya 16 bora michuano ya Antwerp ATP inayofanyika nchini Ubeligiji.

Mshindi huyo wa Grand Slam mara tatu, alikuwa akiongoza 4-1 katika seti ya kwanza, na baadaye aliruhusu Muajentina huyo kurudi na kushinda michezo mitano mfululizo kwa seti 6-4 7-6 (8-6).  na kumtupa nje Andy Murray.

Murray alimtoa Frances Tiafoe katika hatua ya 32 bora na kuibua hisia kubwa katika mechi yake na Schwartzman, akionyesha dalili za kurudi katika ubora wake, ambao alikuwa nao kwa miaka ya nyuma.

“Sikufanya maamuzi mengi mazuri kama vile ningependa katika seti ya pili, kushughulikia mapungufu yangu,” Murray alikubali baada ya kushindwa.

“Mchezo ni biashara ya matokeo. Ukicheza vizuri au vibaya, haijalishi ikiwa utapoteza mechi,” Murray alielezea.

Chanzo: eatv.tv