Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Nick Kyrgios kuzikosa Grandslams zote

Nick Kyrgios Nick Kyrgios.

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mcheza tenisi rai wa Australia, Nick Kyrgios ametangaza kuwa hatashiriki kwenye fainali za michuano ya wazi ya Australia (Australian Open) kutokana na mwili wake kutokuwa tayari kwa ajili ya michuano hiyo.

Ameweka wazi kuwa atarejea pindi mwili wake utakapokuwa tayari kwa ajili ya kucheza michezo ya ushindani.

Kutokana na majeraha yanayamsumbua Kyrgios yalimfanya kutoshiriki kwenye Grandslams zote za mwaka uliopita 2023, alikosa michuano ya wazi ya Australia, ya Marekani (US Open), Ufarana (French Open) na ile ya Wimbledon ambayo hufanyika Uingereza.

Kwa mwaka 2023 raia huyo wa Australia alianza kwa kupata majeraha ya goti ambalo baada alifanyiwa upasuaji, baada alipata maumivu ya mguu na majeraha ya mbavu, ambayo yalimfanya akose minchezo mingi kwenye kalenda ya mwaka 2023.

Kyrgios ana umri wa miaka 28 ambaye ni mwana fainali wa Wibledon mwaka 2022, hajawahi kushinda taji binafsi kwenye michezo ya Grandslams kwa sasa anashika nafasi ya 13 kwa ubora kwenye viwango vya tenisi upande wa wanaume.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live