Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Nadal na Mawazo ya kuvunja Record Australian Open

Rafael Nadal Rafael Nadal afikiria kuweka rekodi

Fri, 28 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rafael Nadal kwa sasa anafikiria zaidi kushinda taji la Australian Open ili aweze kuwa mchezaji namba moja mwenye Grand slam 21 na kuwapita Novak Djokovic na Roger Federer kwenye listi ya wachezaji wenye mataji mengi zaidi kwa muda wote.

Leo Ijumaa Nadal anatarajia kucheza mchezo wake wa nusu fainali na Barrettini, huu ndio mtihani wake wa kwanza ambao atabidi aupitie ili aweze kutimiza azma yake katika michuano ya Australian Open.

Rafael Nadal hajashinda taji la Australian Open tokea mwaka 2009, kwa sasa hii ndio nafasi yake adhimu ya kuweza kushinda taji hilo kwani kutokuwepo kwa Djokovic na Federer kunampa nafasi kubwa ya kuweza kunyakuwa taji hilo.

Djokovic alitolewa kwenye mshindano hayo baada ya kutokidhi masharti ya kuingia nchini Australia kutokana na kanuni za chanjo ya Uviko-19, wakati Federer bado anauguza majeraha yake ya goti na anatarajia kuwa nje zaidi kwa miezi kadhaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live