Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Nadal atinga Nusu Fainali Australian Open

Rafael Nadal Rafael Nadal

Tue, 25 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashindano ya Australian Open 2022 yanaendelea kunoga, hatua ya nusu fainali hiyo kurindima. Rafael Nadal, ndani ya nyumba.

Licha ya kuhitajika kuvishinda vikwazo vingi uwanjani, Nadal amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya ushindi dhidi ya Denis Shapovalov. Huu ni mchezo ambao ulihitaji seti 5 kuamua bingwa kati ya wawili hawa.

Baada ya matokeo ya seti 6-3 6-4 4-6 3-6 6-3, Rafael amefanikiwa kufika hatua ya nusu fainali ambapo, atachuana na mshindi kati ya Matteo Berrettini na Gael Monfils.

Endapo Rafael atafanikiwa kutwaa ubingwa mwaka huu, itakuwa ni ubingwa wake wa 21 wa Grand Slam na, atawapiku wapinzani wake wa muda wote – Novak Djokovic na Roger Federer.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live