Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Nadal amchapa Djokovic robo fainali, French Open

Farael Nadal Rafael Nadal ameshinda kwa mara ya 29 dhidi ya Novak Djokovic

Wed, 1 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mcheza tenisi raia wa Hispania Rafael Nadal amemvua ubingwa wa michuano ya wazi ya Ufaransa (French Open) Novak Djokovic kwa kumfunga kwenye mchezo wa robo fainali usiku wa kuamkia leo.

Nadal ambaye ni bingwa mara 13 wa michuano hii ameshinda mchezo huo kwa seti 3-1 kwa ushindi wa seti 6-2 4-6 6-2 7-6 mchezo uliochezwa kwa masaa 4. huu pia ni ushindi wa 29 kwa Nadal dhidi ya Djokovic kwenye michezo 59 waliokutana huku Djkovic akiwa ameshinda mara 30.

katika hatua ya nusu fainali Rafael Nadal atacheza dhidi ya Alexander Zverev siku ya ijumaa, Zverev ametinga hatua ya nusu fainali kwa kumnyuka Carlos Alcaraz kwenye mchezo war obo fainali kwa seti 6-4 6-4 4-6 7-6 (9-7).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live