Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Nadal ajitoa michuano ya Wazi Australia

Nadal.jpeg Rafael Nadal

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kukaa nje kwa takriban mwaka mzima akiuguza majeraha ya nyonga, mcheza tenisi, Rafael Nadal ameumia misuli ya paja na kuamua kujitoa kwenye michuano ya Wazi ya Australia inayoendelea huko Brisbane, Australia.

Nadal (37) aliwashinda Dominic Thiem na Jason Kubler kwenye mfululizo wa michezo yake tangu aliporejea uwanjani kwenye michuano hiyo ya Brisbane.

Hata hivyo, kwenye mchezo dhidi ya Jordan Thompson alipata majeraha hayo ya misuli ya paja yaliyomlazimu kujitoa kwenye michuano hiyo na alihitaji huduma ya kwanza kuangalia jeraha hilo baada ya seti ya tatu.

Mshindi huyo wa mataji 22 ya Grand Slam alithibitisha kujitoa kwake kwenye michuano hiyo, akikiri anaamini majibu ya majeraha aliyopata 'ni 'habari njema' kwani hayajahusiana na jeraha la nyonga lililomweka nje kwa mwaka mzima.

Aliandika kwenye mtandao wa kijamii; "Habari wote, wakati wa mchezo wangu wa mwisho Brisbane, nilipata tatizo kidogo kwenye misuli ya paja na kama mnavyojua ilinishtua.

"Mara tu nilipofika Melbourne, nilipata nafasi ya kufanya vipimo vikubwa (MRI) na vya misuli, tatizo hilo haliko katika sehemu ambayo niliumia mwanzo, hizo ni habari njema."

"Kwa sasa, sitaweza kushindana kwa kiwango kikubwa kwenye seti tano. Ninarudi Hispania kuonana na daktari wangu, kupata matibabu na kupumzika."

Nadal ambaye alitarajiwa kurudi kwake na kuendeleza ubabe kwenye tenisi, ameshindwa kufanya hivyo na mwenyewe amekiri; "Nilifanya jitihada kubwa kipindi cha mwaka mmoja kwa ajili ya kurudi upya huku na nilishaeleza malengo yangu ni kuwa kwenye ubora wangu katika miezi mitatu.

"Nilitamani kucheza hapa Australia na nimepata kucheza baadhi ya mechi zilizonifanya nijisikie furaha na kuwa imara. Hata hivyo, asanteni kwa sapoti yenu na tutaonana muda si mrefu."

Chanzo: Mwanaspoti