Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Murray hatihati kucheza Wimbledon

Skysports Tennis Andy Murray 6589541 Andy Murray

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kabla ya kuumia na kufanyiwa upasuaji wa mguu wake wa kulia, nyota Andy Murray amebaki njiapanda kama atawahi muda wa kushiriki michuano ya wazi ya kwao Uingereza, Wimbledon inayoanza mapema mwezi ujao.

Murray, bingwa mara tatu wa mataji makubwa ya tenisi duniani (Grand Slam) alishaweka wazi kutumia michuano hiyo kuwa ya mwisho kwake kabla ya kutangaza kuachana na mchezo wa tenisi na kusababisha waandaaji wa michuano hiyo kuandaa utaratibu maalum wa kumuaga.

Michuano hiyo itaanza Julai Mosi na Murray aliyewahi kushinda taji hilo mara moja, anakimbizana na muda kabla pia ya kujua hatma yake ya kuagwa kabla ya kwenda kumalizia tenisi yake kwenye michuano ya Olimpiki Ufaransa kabla ya kustaafu rasmi.

Chanzo: Mwanaspoti