Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Medvedev Ashindwa Kulipa Kisasi kwa Nadal

Nadal Rev Medvedev Ashindwa Kulipa Kisasi kwa Nadal

Sat, 26 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mcheza tennis namba moja kwa ubora duniani Daniil Medvedev ameshndwa kulipa Kisasi kwa Rafael Nadal baada ya kupoteza tena kwa mfululizo wa set 6-3, 6-3 siku ya ijumaa kwenye mchezo wa nusu fainali kwenye mashindano ya Mexico Open.

Medvedev alipoteza kwenye mchezo wa fainali ya Australian Open dhidi ya Nadal, ambapo nyota huyo kutoka nchini hispania alifanikiwa kutoka nyuma baada ya kuongozwa kwa set mbili kwenye mchezo ambao ulichezwa kwa set tano.

Medvedev ambaye alishika namba moja, baada ya nyota wa Serbia Novak Djokovic kupoteza kwenye mchezo wa robo fainali kwenye mashindano ya Dubai siku ya alhamisi.

Rafael Nadal kwa sasa anaenda kucheza fainali ya Acapulco huku akiwa anaenda kupigania taji lake la nne, taji lake la kwanza alichukua 2005 na la pili 2013 wakati mashindano hayo yanachezwa kwenye udongo na taji lake la tatu alishinda mwaka 2020 baada ya kuamishiwa kwenye uwanja sakafu ngumu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live