Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Matteo Berrettini Bingwa Stuttgart Open

Matteo   Bossssss Matteo Berrettini Bingwa Stuttgart Open

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Andy Murray amekosa taji lake la kwanza la uwanja wa nyasi tangu ashinde Wimbledon mnamo 2016 baada ya kufungwa na Matteo Berrettini katika Fainali ya Stuttgart Open leo jana Jumapili.

Mchezaji huyo namba moja wa zamani alikumbana na kichapo cha 4-6 7-5 3-6 kutoka kwa Muitaliano huyo katika kile kilichokuwa ni kipigo chake cha pili katika fainali 10 za uwanja wa nyasi.

Pengine wasiwasi mkubwa zaidi ulikuwa kwa Murray kuhitaji matibabu kutoka kwa physio mara mbili katika seti ya tatu.

Berrettini alikuwa akicheza katika mchuano wake wa kwanza tangu Machi kutokana na jeraha la mkono wa kulia ambalo lilimweka nje wakati wa msimu wa udongo.

“Imekuwa wiki ya kuvutia. Niliifurahia sana. Ningependa kumpongeza Matteo na timu yake kwa wiki nzuri,” Murray alisema katika mahojiano

“Amerejea kutoka kwenye upasuaji na si rahisi. Alicheza vizuri sana leo na alistahili ushindi. Hatimaye, asante kwa timu yangu hapa na timu yangu nyumbani.” aliongeza Murray

Chanzo: www.tanzaniaweb.live