Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Magwiji waendelea kuaga mashindano - Wimbledon

RADDU Emma Raducanu

Fri, 1 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Magwiji wa Tennis wameendelea kufungashiwa virago katika michuano ya wazi ya Wimbledon inayofanyika nchini England baada Emma Raducanu na Andy Murray kuungana Serena Williams kuaga michuano hiyo.

Emma Raducanu alizidiwa nguvu na Caroline Garcia wa Ufaransa katika mchezo wa mzunguko wa pili wa michuano hiyo na kukubali kichapo cha seti mbili mfululizo kwa alama cha 6-3 na 6-3. Raducanu mwenye umri wa miaka 19 amesema hakuwa na matarajio ya kufanya vizuri sana kwenbye michuano hiyo kwani bado hana muda mrefu tangu apone majeraha.

Andy Murray

Naupande wa Bingwa mara mbili wa Wimbledon Andy Murray naye alionyeshwa mlango wa kutokea baada ya kufungwa seti nne na John Isner katika mchezo mzungi wa pili.

Isner raia wa marekani alipata ushindi wa kwanza dhidi ya MScotish huyo katika mchezo wao wa tisa kukutana, akipiga aces 36 katika ushindi wa alama 6-4 7-6 (7-4) 6-7 na (3-7) 6-4. Murray alifanikiwa kupata alama 15 tu dhidi ya Isner katika mchezo huo.

Katika mzunguko wa kwanz amichuano hiyo nyota mwenye grandlsam 23 lwa wanawake Serena Williams alitupwa nje ya michuano hiyo ya wazi ya Wimbledon na Mfaransa Harmony Tan kwa seti alama 7-5,1-6,7-6 na (10-7).

Baada ya kupoteza mchezo huo Serena amesema bado hajajua hatma yake kama atastaafu kucheza tennis ama ataendelea kuisaka rekodi ya nyota wa zamani wa Australia Margaret Court anayeshikilia rekodi ya kutwaa mataji 24 ya Gland Slam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live