Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Konta atupwa nje Miami Open

05d0cf56b2fb6d767719fe4b46cc1080 Konta atupwa nje Miami Open

Mon, 29 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MWINGEREZA, Johanna Konta ametupwa nje ya michuano ya Miami Open baada ya kufungwa na mchezaji namba tisa duniani katika mchezo wa teni kutoka Jamhuri ya Czech, Petra Kvitova katika raundi ya tatu ya michuano hiyo.

Konta anayeshika nafasi ya 17 kwa sasa alipoteza mechi hiyo kwa 6-1 6-2 kwa dakika 58 dhidi ya bingwa mara mbili wa Wimbledon Kvitova.

Kvitova hakupata hata kupumua dhidi ya Mwingereza namba moja Konta aliyeshinda taji la Miami mwaka 2017.

Sasa atacheza na mchezaji namba tano Elina Svitolina mechi ya robo fainali baada ya mchezaji huyo wa Ukraine kumfunga Ekaterina Alexandrova kwa 7-6 (7-1) 6-4.

Victoria Azarenka alimfunga Angelique Kerber kwa 7-5 6-2 na kutinga raundi ya nne ambapo sasa atacheza na mchezaji namba moja wa zamani Ashleigh Barty.

Bingwa mtetezi Barty, ambaye ataendelea kubaki kileleni kwa ubora wa viwango kama atafuzu fainali za michuano hii, alimfunga Jelena Ostapenko kwa 6-3 6-2.

Mchezaji namba tatu Simona Halep alijitoa kwenye mechi yake dhidi ya Anastasija Sevastova kutokana na kuumia bega.

Chanzo: www.habarileo.co.tz