Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Djokovic ruksa kutetea Wimbledon Open 2022

217355399 3934436216679383 67820893314248759 N Nyota wa tennis Novak Djokovic akishikilia taji la Wimbledon 2021

Wed, 27 Apr 2022 Chanzo: eatv.tv

Bingwa wa michuano ya wazi ya Wimbledon 2021 Mserbia Novak Djokovic atatetea ubingwa wake kwenye mashindano ya mwaka huu baada ya waandaaji wa mashindano hayo kuweka wazi washiriki wa michuano hiyo sio lazima wawe wamechanjwa chanjo ya Uviko 19.

Djokovic mwenye umri wa miaka 34 ambaye anashika nafasi ya kwanza kwa viwango vya ubora wa tennis duniani alishindwa kushiriki kwenye michuano miwili ya Australian Open 2022 na mashindano ya Indian Wells sambamba na ATP Miami  Masters 2022 yaliyofanyika mjini California nchini Marekani.

"vigezo vilivyowekwa na serikali kuingia nchini Uingereza havilazimishi watu kuchoma chanjo ya uviko 19,japo wanasisitiza kupata chanjo lakini sio jambo la lazima kwa mtu kuweza kuchanja”amesema mtendaji mkuu mashindano hayo Sally Bolton.

Sasa Djokovic maarufu kama Joker atakuwa anatafuta taji lake la 21 la Grand Slam kwenye mashindano ya Wimbledon 2022 yanayotarajiwa kuanza mnamo June 27 na kumalizika July 10, 2022 nchini Uingereza.

Chanzo: eatv.tv