Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Djokovic kulipa kisasi kwa Zverev US Open

Novac Djocovic Mcheza Tennis, Novac Djokovic

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bingwa nambatri moja Duniani wa mchezo wa Tennis Novak Djokovic ataendelea kuwania Grand Slam ya nne mwaka huu atakapovaana na bingwa wa Olimpiki Alexander Zverev katika mchezo wa nusu fainali ya US Open utakaopigwa siku ya Ijumaa.

Mbabe huyo mwa tennis Duniani amefuzu nusu fainali baada ya kumnyuka Matteo Berrettini kwa seti 5-7, 6-2,6-2,6-3 .

Zverev ambaye anashikilia nafasi ya nne kwenye viwango vya ubora Duniani ndiye aliyeizima ndoto ya Djokovic katika michuano ya Olimpiki baada ya kumtupa nje katika nusu fainali.

Iwapo Djokovic atashinda US Open atakamilisha kibindoni Grand Slam ya nne baada ya kufanikiwa kutwaa Australian Open, French Open na Wimbledon mapema mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live