Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Djokovic hakamatiki Paris Masters

Https   Cdn.cnn .com Cnnnext Dam Assets 211107112631 Djokovic Paris Masters Novak Djokovic

Mon, 8 Nov 2021 Chanzo: eatv.tv

Nyota wa mchezo wa tenisi Mserbia Novak Djokovic atamaliza mwaka huu akiwa namba moja kwenye viwango vya ubora kwa mara ya saba ikiwa ni rekodi kufuatia kutwaa taji la Paris Masters alipomshinda Daniil Medvedev katika fainali.

Djokovic alipoteza seti ya kwanza kwa 6-4 kabla ya kuibuka kidedea kwa seti mbili mfululizo 6-3, 6-3.

Taji hilo lilikuwa ni taji la 6 la Djokovic katika michuano ya Paris Masters na ni la 37 kwenye fainali za ATP Tour Masters huku akiweka rekodi kuwa ndiye mchezaji mwenye mataji mengi zaidi ya masters akimpiku Rafael Nadal mwenye mataji 36.

Mrusi Medvedev na Djkovic wote watashiriki kwenye Michuano ya ATP Tour huku Turin Italia itakayoanza November 14 ambayo ndio mashindano ya mwisho kwenye kalenda ya mwaka.

Chanzo: eatv.tv