Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Djokovic atamani medali ya dhahabu Paris 2024

Nova Nyota wa tennis Novak Djokovic

Fri, 18 Feb 2022 Chanzo: eatv.tv

Nyota wa tennis kutoka Serbia Novak Djokovic amesema malengo yake kwa sasa ni kunyakua medali ya dhahabu kwenye michezo ya olympic inayotarajiwa kufanyika mnamo mwaka 2024 mjini Paris nchini Ufaransa .

Djokovic 34, ambaye anakamata nafasi ya kwanza kwa ubora wa viwango vya ubora wa tennis kwa upande wa wanaume aliondolewa katika hatua ya nusu fainali kwenye michezo ya olympic iliyofanyika mjini Tokyo mwaka 2020 na Mjerumani Alexander Zverev kabla ya kufungwa tena na Mhispania Pablo Carreno Busta na kukosa hata medali ya shaba kutoka nchini Japan.

"medali ya Olympic hasa ya dhahabu ni kitu cha thamani na ndicho ninachowaza,bahati mbaya sikupata nafasi ya kuipambania kwenye michezo iliyopita ya Olympic lakini natazamia kuwepo mjini Paris mwaka 2024 kushiriki" amesema Djokovic

Novak Djokovic ambaye anatarajiwa kurejea kwenye ulingo wa tennis wiki ijayo kwenye mashindano ya ATP 500 Dubai Tennis Championships ambayo hayana vikwazo vya chanjo ya covid 19 huku michuano hii itakuwa ya kwanza kwa Djokovic tangu azuiliwe nchini Australia kwenye mashindano ya Australian open na mwenyewe kusema vyote vilivyotokea mwaka huu havikutarajiwa na ni ngumu kuweza kusahau lakin atarejea tena nchini Australia kwa siku za mbeleni nakucheza ndani ya Rod Laver Arena (akimaanisha kushiriki mashindano ya Australian open )

Chanzo: eatv.tv