Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Djokovic ajitoa Shanghai Masters

Novak Djokovic Walter Mchezaji namba moja kwa ubora kwenye mchezo wa tennis Duniani Novak Djokovic

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji namba moja kwa ubora kwenye mchezo wa tennis Duniani Novak Djokovic hatashiriki michuano ya tennis ya Shanghai Masters 2023.

Djokovic ametangaza kuwa hata shiriki michuano hii kupitia mitandao ya kijamii. Shanghai Masters inarejea mwaka huu kwa mara ya kwanza tangu 2019.

Djkovic ndio bingwa wa muda wote wa michuano hii akiwa ameshinda ubingwa wa Shangai Masters mara 4, ameandika kupitia mtandao wa X kuwa hatakuwa sehemu ya michuano hii mwaka huu 2023.

"Kwa miaka mingi, baadhi ya msaada bora ninaopokea popote Duniani ni China. Shanghai imekuwa moja ya mashindano yangu bora katika msimu. Nitakosa #NoleFam yangu nchini China. Natumai kwamba nitarudi China katika siku zijazo na kucheza mbele yenu tena." Ameandika Djokovic kwenye mitandao ya kijamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live