Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Djokovic Agomea Chanjo, Kukosa Wimbledon na French Open

Novak Djokovic1 Mcheza Tennis, Novac Djokovic

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mcheza Tenisi namba moja kwa ubora duniani, Novak Djokovic anasema hayupo kinyume na chanjo lakini hataweza kutetea taji lake la Wimbledon au French Open ikiwa atalazimishwa kuchanjwa chanjo ya Covid-19.

Djokovic, ambaye hajachanjwa, alifukuzwa kwenye Australia Open kabla ya Grand Slam ya kwanza ya mwaka baada ya siku 11 kufuatia kufutwa kwa visa mara mbili, changamoto mbili za mahakama na usiku tano katika hoteli ya kizuizini ya wahamiaji.

“Sijawahi hata siku moja kupinga chanjo,” aliiambia BBC, “lakini siku zote nimeunga mkono uhuru wa kuchagua unachoweka mwilini mwako.”

Licha ya kumtazama mpinzani wake, Rafael Nadal, akishinda taji la 21 la rekodi la Grand Slam mjini Melbourne mwezi uliopita, mchezaji nambari 1 wa dunia anasema hatatetea mataji yake ya Wimbledon au French Open ikiwa mashindano yanahitaji chanjo ya lazima kwa washindani.

“Ndiyo, hiyo ndiyo bei ambayo niko tayari kulipa,” Djokovic alisema alipoulizwa kama angejitolea kushiriki mashindano hayo.

“Ninasema kwamba kila mtu ana haki ya kuchagua au kutenda au kusema au kuhisi chochote kinachofaa kwake.”

“Kanuni za kufanya maamuzi juu ya mwili wangu ni muhimu zaidi kuliko taji lolote au kitu kingine chochote. Ninajaribu kuwa sawa na mwili wangu kadri niwezavyo.” aliongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live