Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Denis Shapovalov akutwa na maambukizi ya Uviko-19

Teneesee Denis Shapovalov

Sun, 26 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji nyota wa tenisi kutoka nchini Canada Denis Shapovalov amethibitishwa kuwa na maambukizi ya Uviko-19 baada ya kupimwa alipotua jijini Sydney nchini Australia alipokwenda kushirika masshindano ya ATP Cup.

Denis Shapovalov ni moja ya wachezaji wa kwanza kuwasili Australia na kugundulika kuwa na maambukizi, wiki iliyoisha alikuwa anashiriki mashindano ya “Tennis Championship exhibition” kwenye nchi za falme za kiarabu jijini Abu Dhabi ambapo alimtoa mchezaji bora Rafael Nadal.

Shapovalov alichapisha chapisho kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akisema kuwa amejitenga na alikuwa na dalili za kawaida tu.

“Habari, nilikuwa nataka kutoa taarifa ya kuwa nimefika sydney, na nimepimwa nimekutwa nina maambukizi ya Uviko-19, kwa sasa nafwata taratibu zote ikiwemo kujitenga na nilikuwa nataka kuwajulisha wote niliokuwa nao wajue.

“Kwasasa nina dalili za kawaida natumai kupona haraka na kurudi uwanjani nitakapo kuwa nimepona kabisa.” Alisema Denis Shapovalov.

Wachezaji wote inabidi wapimwe na kwa usalama na wawe hawana maambukizi kwa saa 72 kabla kusafiri kwenda Australia na pia watapimwa tena watakapofika nchini humo na kujitenga wakisubiri majibu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live