Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Bingwa Us Open apata Covid-19

EMMA Emma Raducanu

Tue, 14 Dec 2021 Chanzo: eatv.tv

Bingwa wa michuano ya tennis ya US Open, Mwanadada Emma Raducanu ana matumaini atarejea kwenye michuano ya tennis ya Australian Open baada ya kupata maambukizi ya Uviko 19 na kujiondoa kwenye michuano ya Mubadala World Tennis Championships inayotarajiwa kuanza December 16-18 mjini Abu Dhab

Raducanu mwenye miaka 19, alipangwa kucheza na bingwa wa medali ya dhahabu ya Olympic  Bellinda Bencic kwenye michuano hiyo mjini Abu Dhabi na sasa atasubiri kushiriki kwenye michuano ya WTA Melbourne ili kujiweka sawa kabla ya kushiriki kwenye michuano ya wazi ya Australia.

"Nilitamani  kucheza mbele ya mashabiki hapa Abu Dhabi, na nimejitenga kufuata sheria na matumaini yangu nitarejea muda sio mrefu” Amesema Raducanu.

Emma Raducanu anayekamata nafasi ya kwanza kwa ubora kwa nchini England aliweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa taji kubwa la tennis (Grand Slam)  la US Open kutokea kufuzu mpaka kwenda kubeba taji hilo na sasa ananolewa na kocha mpya Torben Beltz.

Chanzo: eatv.tv