Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Barty aliniliza kwa dakika 40- Swiatek

Igaaaaaaa Nyota wa tennis Iga Swiatek

Mon, 4 Apr 2022 Chanzo: eatv.tv

Nyota wa tennis Mpoland Iga Swiatek amesema alipatwa na mshangao baada ya kusikia taarifa za bingwa wa Australian Open 2022 Muastralia Ashleigh Barty kutangaza kuachana na mchezo wa tennis kwani kitendo hicho hakukitegemea kutokea kwa siku za hivi karibuni

Swiatek mwenye umri wa miaka 20 ambaye kwa sasa anakamata nafasi ya kwanza kwa ubora wa viwango vya ubora duniani kwa upande wa wanawake na kuwa Mpoland wa kwanza kukamata nafasi ya hiyo ya juu duniani kwa viwango vya tennis.

"nililia kwa dakika 40 sababu sikujua kwa nini Ashleigh Barty  ameamua kujiuzulu mana sikujua kama ni kitendo ambacho kingeweza kutokea mapema ilinishangaza sana . Siku zote nilikuwa na mawazo ya sisi wote kushindana mpaka tukifikisha miaka 35 na kuendelea lakini kwa sasa haiwezekani tena “ amesema Swiatek

Mpaka sasa Swiatek amecheza michezo 17 bila ya kupoteza huku akishindi mataji matatu ya WTA kwa mwaka 2022 huku akiingia kwenye rekodi za kuwa mchezaji wa nne kutwaa mataji mawili ya Indian Wells na Miami Open kwenye rekodi za mashindano hayo huku akichukua nafasi ya kwanza kwa viwango vya tennis akichukua nafasi ya Ashleigh Barty aliyejiuzulu kucheza mchezo huo . 

Chanzo: eatv.tv