Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Barty ajiondoa michuano ya Miami Open

Ashely Barty Nyota wa tennis Ashely Barty

Fri, 4 Mar 2022 Chanzo: eatv.tv

Nyota wa tennis Muaustralia Ashleigh Barty amejiondoa kwenye mashindano yanayokuja ya Indian Wells Masters na Miami Open kwa kuwa amekosa maandalizi ya kutosha kueleka kwenye mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza mnamo March 7 mpaka March 20 mjini California nchini Marekani

Barty mwenye umri wa miaka 26 ambaye anakamata nafasi ya kwanza kwa viwango vya ubora duniani upande wa wanawake aliweka rekodi ya kutwaa taji la wazi la Australian 2022 ikiwa ni miaka 44 kupita kwa mchezaji mzawa kutoka Australia kutwaa taji hilo tangu mwaka 1974.

"kwa kweli mwili wangu bado haujakaa sawa tangu nishinde taji ya wazi la Australian 2022 na sikuwa na maandializi ya kutosha kwa hiyo siamini kama nitaweza kushinda mashindano haya matokeo yake imenilazimu kujiondoa kwenye michuano yote miwili "amesema Barty.

Ashley Barty sasa anaungana na mwanafainali mwenzake wa Australian Open 2022 Mmarekani Danielle Collins ambaye na yeye amejiondoa kwenye fainali hizo mbili za Indian Well Masters na Miami Open kutokana na majeraha huku Barty akitarajiwa kurejea kwenye mashindano ya Billie Jean King Cup kuiwakilisha Australia mnamo mwezi April 2022.

Chanzo: eatv.tv