Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Australian Open: Ushiriki Wa Djokovic Ni Gumzo.

NOvak Djikovic Vv Novak Djokovic

Sat, 8 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati muda ukiyoyoma kuelekea mashindano ya Australian Open, Januari 10,2022. Ushiriki wa bingwa mtetezi, Novak Djokovic, ni gumzo duniani.

Djokovic anaingia kwenye headlines za michezo na siasa duniani kwa kitendo cha uongozi wa Melbourne kusitisha visa ya mchezaji huyu ambaye ni bingwa mtetezi wa mashindano ya Australian Open na pia, ni mchezaji namba 1 kwa ubora duniani (wanaume).

Sababu ya kusitishwa kwa visa ya Djokovic imekuwa ni gumzo. Hii ni baada ya serikali ya Australia kumpatia kibali maalumu cha kuingia nchini humo bila kuwa na ulazima wa kuchanja chanjo dhidi ya COVID-19. Lakini, baada ya kuingia nchini humo, Djokovic amejikuta akiishia uwanja wa ndege na kuchukuliwa na maafisa uhamiaji ambao wamemueka kwenye hoteli yao maalumu.

Kuzuiliwa kwa Djokovic kuendelea na maandalizi yake ya kutetea taji la Australian Open, kumezua taharuki miongoni mwa mashabiki na wananchi kote duniani. Baadhi ya wananchi wa Australia hawajapendezeshwa na kitendo cha serikali kumruhusu Djokovic kuingia nchini huku akiwa hajulikani kama amachanja au hajachanja.

Kitendo hichi kimetafsiriwa kama usaliti wa serikali kwa wananchi wake. Hii inatokana na sheria iliyowekwa nchini humo ambayo, hairuhusu mtu yeyote kuingia nchini bila kuwa na uthibitisho wa kuchanja au kutochanja.

Wengine wameenda mbali sana (hasa mashabiki wa Djokovic na serikali ya nchini Serbia) na kudai kuwa, wanachomfanyia Djokovic ni uzalilishaji na hivyo, mamlaka zinazohusika, zimuachie mchezaji huyo haraka iwezekanavyo. Gumzo hili linaiweka Australia (kama nchi) kwenye mjadala wa kisiasa (ndani ya nchi) na kidiplomasia (na mataifa mengine, Serbia ikiwa ni muhusika).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live