Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Australian Open 2022: Osaka Anawaka

Qbeqknf8 Naomi Osaka Afp 625x300 17 January 22 E1642417232319 768x516 Naomi Osaka

Tue, 18 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati headlines za Djokovic vs Serikali ya Australia zikiwa zimetamatika, mashindano ya Australian Open 2022 yameanza rasmi siku ya jana. Naomi Osaka ameanza kwa kishindo.

Bingwa mtetezi wa Australian Open (wanawake), Naomi Osaka, ameyaanza vyema mashindano ya mwaka huu kwa ushindi kwenye mchezo wa kwanza. Osaka alikuwa uwanjani kuchuana na Camila Osorio mchana wa siku ya jana.

Osaka alianza vyema mchezo kwa kuongoza kwa matokeo ya 5-0 kabla ya Osorio kupindua meza. Uwepo wa mashabiki uwanjani, ubora binafsi na upinzani kutoka kwa Osorio, vilimuongezea ari Osaka ambaye alirejea tena kwenye nafasi ya kuongoza na kumaliza mchezo kwa seti 6-3 6-3.

Wakati Osaka akiibuka kidedea, kwa mara ya pili mfululizo, Sofia Kenin anayaaga mashindano kwenye hatua za mwanzo baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Madison Keys. Kenin ambaye alikuwa bingwa wa Australian Open 2020, amejikuta akiambulia kipigo na kutolewa mapema kwenye mashindano ya mwaka 2021 na 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live