Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Auger-Aliassime bingwa Tennis Rotterdam Open 2022

TENNIS Felix Auger-Aliassime akiwa kwenye mashindano ya Rotterdam Open

Mon, 14 Feb 2022 Chanzo: eatv.tv

Felix Auger-Aliassime amekuwa bingwa wa mashindano ya Tennis ya Rotterdam Open ya Nchini Uholanzi baada ya kumfunga mgiriki Stefano Tsitsipas anayeshika nafasi ya nne kwenye viwango vya ubora Duniani kwa seti 2-0.

Felix (21) anayeshika nafasi ya tisa kwenye viwango vya ubora Duniani ameshindwa kwa 6-4, 6-2 katika mchezo uliodumu kwa dakika 78. Ushindi huo ni wa kwanza kwa nyota huyo baada ya kupoteza fainali 8 mfululizo.

Baada ya Ubingwa huo, Felix amesema “Ni siku ya furaha sana kwenye maisha yangu ya Tennis na ninaimani ni mwanzo wa makombe mengi yanayokuja”.

Nyota huyo raia wa Canada alitabiriwa makubwa baada ya kuwatoa vigogo wa England, Cameroon Norrie na Andy Murray kwenye michezo ya hatua za mwisho za mtoano wa mashindano hayo.

 

Chanzo: eatv.tv