Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Ashleigh Barty kustaafu Tennis

ASH Bingwa wa michuano ya Tennis Australian Open, Ashleigh Barty

Wed, 23 Mar 2022 Chanzo: eatv.tv

Bingwa wa michuano ya Tennis Australian Open, Ashleigh Barty ametangaza kustaafu kucheza tennis atakapotimiza umri wa miaka 25 April 24 mwaka huu huku akisema sababu ya kufikia uamuzi huo ni kutaka kutimiza ndoto zake nyingine nje ya mchezo huo.

Barty amesema “Nina furahia na nipo tayari kwa ajili ya uamuzi huo. Kutoka moyoni, ni uamuzi sahihi. Naelewa watu hawatonielewa. Ni sawa, kwasababu najua Ash Barty ana ndoto nyingi ambazo anataka kuzitimiza hivyo sio lazima awe ana safari sana, kuwa mbali na familia, mbali na nyumbani  ambapo siku zote ningependa kuwepo”

Ashleigh ambaye anashika nafasi ya kwanza kwenye viwango vya ubora duniani kwa wanawake, ameshinda mataji matatu ya Grand Slam ambayo ni Tennis French Open mwaka 2019, Tennis Wimbledon 2021 na Tennis Australian Open January 2022.

Chanzo: eatv.tv