Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Ashleigh Barty Bingwa Australian Open 2022

Austr Open Ashleigh Barty atwaa ubingwa wa Australian Open

Sat, 29 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yametimia, baada ya miaka 44, Ashleigh Barty anakuwa raia wa kwanza wa Australia kutwaa ubingwa wa Australian Open.

Barty ameibuka kidedea baada ya kumfunga Danielle Collins kwa matokeo ya seti 6-3 7-6 7-2 ukiwa ni mchezo ambao ulitawaliwa na upinzani mkubwa.

Ashleigh Barty alianza kwa kuongoza kwenye seti ya kwanza kabla ya Collins kuonesha maajabu yake kwenye seti ya pili kwa kuongoza 4-0. Kuelekea mwishoni mwa seti ya 2, Barty alionesha ubora na uhodari wake uwanjani kwa kushambulia na kusawazisha matokeo kuwa 4-4.

Piga n’kupige ziliendelea kwenye seti ya pili mpaka matokeo kuwa 7-6 na mchezo kuamuliwa kwa tie break na champion set ambazo, Barty alishinda kwa matokeo ya 7-2.

Ushindi wa Barty unakuwa ni ushindi wake wa 3 wa Grand Slams huku Collins akiwa kwenye nafasi kubwa ya kuingia kwenye orodha ya wachezaji 10 bora duniani (kwa wanawake) mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live