Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Andy Murray atolewa Kwenye Mashindano ya Madrid Open

Andy Murray Ruled Out.jpeg Andy Murray atolewa Kwenye Mashindano ya Madrid Open

Fri, 6 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa mchezo wa tennis Andy Murray ameondolewa kwenye mashindano ya Madrid Open kwenye mzunguko wa tatu ambapo alitakiwa kukutana na Novak Djokovic kwa sababu ya ugonjwa.

Ni bahati mbaya kwa Andy Murray ambaye ametoka kushinda kwenye mchezo dhidi ya Denis Shapovalov siku ya jumanne ambapo alifanikiwa kushinda baada ya kuongozwa kwa set kadhaa na alikuwa anajiandaa kukutana na mpinzani wake wa muda mrefu.

Ujumbe ulichapishwa kwenye ukurasa wa Tweeter ulisomeka, “Kwa bahati mbaya, Andy Murray hataweza kuwepo kwenye uwanja wa Manolo Santana kutokana na ugonjwa. tunamtakia heri apone haraka.”

Ikiwa atapona haraka Andy Murray ataamua kama atacheza michezo ya kufuzu wiki ijayo kwenye mashindano ya Italian Open, huku wakati mashindano ya French Open yakiwa bado muhimu kwake japo kuwa awali alisema hata shiriki badala yake atajikita kujiandaa na msimu wa “grass-court”.

Andy Murray amesaidia kuweka historia kwa waingereza kwenye nchi ya hispania kwa mchezo wa tennis, akiungana na Dan Evans na Cameron Norrie kwa kuwa miongoni mwa wachezaji walifika kwenye mzunguko wa tatu kwenye mashindano sawa kwenye viwanja vya udongo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live