Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Andy Murray Atupwa nje Michuano ya BNP Paribas Open

Murray Andy BNP Paribas Open Andy Murray

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mcheza Tenisi namba moja duniani, Andy Murray amepoteza mchezo na kuondolewa rasmi kwenye mashindano ya BNP Paribas Open na Alexander Bublik wa Kazakhstan kwa seti moja kwa moja pale Indian Wells.

Murray alipokea upinzani mkali katika mchezo uliokuwa wa kusisimua katika seti ya kwanza ambao ulienda kwa 11-9 kabla ya Bublik kufunga seti ya pili na kumalizia ushindi wa 7-6 6-3 ndani ya masaa mawili tu.

Murray, ambaye alikuwa ameshinda ushindi wake wa 700 wa ATP Tour kwa kumshinda Taro Daniel katika raundi ya kwanza, alipambana vikali lakini hakuweza kubadili matokeo.

Mchezaji huyo wa Uingereza alianza vyema, ingawa alipoteza nafasi nzuri ya kuongoza seti ya ufunguzi na kushindwa kufanya hivyo akiwa nyuma kwa seti 2-1.

Bublik 24, ambaye anacheza Indian Wells kwa mara ya kwanza, aliimarika zaidi kadiri mechi ilivyokuwa ikiendelea na kufanikiwa zaidi katika mchezo wa nne wa seti ya pili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live